Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji ,Clifford Tandari akizungumza na baadhi ya Watumishi wa Kituo hicho pamoja na Waandishi wa Habari wakati walipotembelewa na balozi wa Israel kuzungumzia Kongamano la Biashara na Uwekezaji litakalofanyika Tel Aviv Israel.
Balozi wa Israel Nchini Tanzania,Yahel Vilan akizungumzia Kongamano hilo ambalo kwa mara ya kwanza litafanyika nchini Israel baada ya kufanyika Tanzania kwa mara ya Tatu mfululizo.
KITUO cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya nchi za nje na Taasisi za Sekta binafsi Tanzania kimeandaa kongamano maalum la kuamasisha na kukuza uwekezaji na biashara kati ya Tanzania na Israel kwa lengo la kuisaidia na kuitangaza tanzania kama ni miongoni mwa maeneo yenye fursa na mazingira mazuri ya kibiashara kwa kampuni nyingi za Israeli.
Kongamano hilo ambalo kwa mara ya kwanza litafanyika nchini Israel baada ya kufanyika Tanzania mara tatu mfulilizo linatarajia kufanyika kuanzia tarehe 28 novemba hadi 30 mwaka huu ambalo litahudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wawekezaji, wafanyabiashara wakubwa na wataalamu mbalimbali huko Tel Aviv Isrel.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji , Clifford Tandari amesema kuwa malengo ya Kongamano hilo ni kutoa fursa za biashara na uwekezaji zilizopo hapa nchini kwa wawekezaji wa Isrel ambazo zipo maeneo katika sekta mbalimbali kama vile viwanda, kilimo na Usindikaji wa mazao,Nishati, Afya,Teknologia, Elimu, Maji ,Majengo,Chakula ,Dawa, Utafiti na Maendeleo.
Bw.Tanadri ametoa two kwa makampuni ya Tanzanania kwenda kushiriki kongamano hilo ili kuanzisha na kukuza ushirikiano katika nyanja za biashara na uwekezaji kwa kushirikiana na Kampuni na wafanyabiashara wa Israel, kwani kuna uwezekano mkubwa Tanzania ikaongeza thamani yake.thamani ya mitaji na uwekezaji kutoka nje iwapo makampuni ya Israel yatakayohudhuria kongamano hilo yataamua kufanya uwekezaji.
"Tunatoa wito kwa makampuni yetu ya Kitanzania yaweze kwenda kushiriki katika kongamano hili maana ni fursa za kipekee sana,” amesema Tandari
Naye Mh.Balozi wa Israel Nchini Tanzania Bw.Yahel Vilan ameeleza kuwa amefurahishwa na kongamano hilo na anaamini kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zitashiriki vizuri Kongamano hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...