Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi mapema leo ameongoza zoezi lakuteketeza bidhaa mbali mbali yakiwamo Madawa ya Binadamu (Drip, Dawa za maumivu), Vyakula, Vipodozi nk...
DC ametekeleza zoezi hilo baada yakuwa amewaagiza watu wa TFDA, kufanya Msako Madukani kuangalia ubora wa Bidhaa.
Ndejembi akizungumza mapema alisema "Niliagiza watu wa TFDA kufanya msako wa Bidhaa zilizokwisha muda wake, Lengo langu nikuhakikisha Kongwa haiwi Kichaka cha Bidhaa zilizokwisha muda wake".
akiwa na Kamati yake ya ulinzi na Usalama Wamesema kuwa Zoezi hilo ni Endelevu ili kukomesha ujanja ujanja wa Wafanya Biashara wasio na Maadili mema ya ufanyaji Biashara.
Sehemu ya Bidhaa hizo zikiwa zimetupwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Deo Ndejembi akiwa na Kamati yake ya Ulinzi la Usalama pamoja na Maafisa wa TFDA.
Wiki moja kabla mngeweza hata kuwapa wagonjwa hospitalini hata kwa nusu bei, au wanafunzi wa mabwenini, wafungwa magerezani, watu masikini ombaomba. Mmeacha tu mpaka tarehe ipite mharibu chakula wakati kuna watu wanalala njaa.
ReplyDeleteMdau uarabuni.