Rais Ali Hassan Mwinyi katika picha ya pamoja na kamati ya Saidi Taifa Stars Ishinde aliyoikaribisha Ikulu jijini Dar es salaam kwa kazi nzuri waliyofanya ya kuwezesha Taifa Stars kunyakua ubingwa wa Challenge Cup ya  Afrika Mashariki mwaka 1994. Toka wakati huo Tanzania haijashinda tena kombe hilo.
Waliosimama mbele toka kulia ni Ankal, Brigedia Moses Nnauye, Mwenyekiti wa chama cha soka (FAT) Alhaj Muhidin Ndolanga, Mhe. Rais, Profesa Philemon Sarungi (wakati huo waziri wa afya), Mwenyekiti wa kamati Mzee Reginald Mengi, Mbunge wa Dodoma Mhe. Kuwayawaya S. Kuwayawaya, na mwanahabari Richard Mwaikenda. 
Nyuma kutoka kulia ni Joseph Senga, Stephen Rweikiza, Deus Mhagale, Kanali Ali Mwanakatwe, Richard Ndassa, Japhet Sanga, Godfrey Lutego, nyuma yao ni Evarist Mwitumba, James Nhende, Meja Jenerali Makame Rashid na nyuma yake ni mwanahabari Edmund Msangi na mwandishi jina limenitoka.
Picha ya chini ni Mwalimu Julius Nyerere akiwa na kikosi cha Timu yetu ya Taifa iliyoshinda kombe la Gossage mwaka 1964 alipowakaribisha Ikulu jijini Dar es salaam kuwapongeza.  
Gossage Cup ni mashindano yaliyoshirikisha timu za taifa za Kenya, Uganda, Tanganyika na  zanzibar. Mechi ya kwanza ilipigwa kati ya kenya na uganda mwaka 1926 ambapo kenya waliibuka washindi kwa bao 3-1 kwa aggregate baada ya kurudiana walipotoka sare mechi ya kwanza. Tanganyika ilishiriki kuanzia mwaka1945 na Zanzibar toka mwaka 1926. Michuano hiyo ilikuwa inadhaminiwa na kampuni ya kutengeneza sabuni ya Gossage, iliyokuwa inamilikwa na ndugu wa kiingereza walioitwa Level Brothers. Tanganyika ilikuja kutwaa kombe hilo mwaka 1964.

Mwaka 1967 jina la michuano hiyo ilibadilika na kuitwa East and Central African Challenge Cup  kabla ya kubadilika kuwa Baraza la vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati Council  of East and Central African Football Associations (CECAFA) ambapo Tanzania ndio walishinda huo mwaka 1994.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...