Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Madaktari wenzao wa Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia wakimfanyia mgonjwa upasuaji wa moyo kwa njia ya kufungua kifua na kuziba tundu la moyo. Kulia ni Dkt. Bingwa wa Upasuaji Hussein Hassan akifuatiwa na madaktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto Dk. Godwin Godfrey (kushoto) na Dkt. Benjamin Bierbach.
Madaktari bingwa wa moyo pamoja na wauguzi kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Nchini Australia wakiendelea na kazi ya kumfanyia mgonjwa upasuaji wa moyo kwa njia ya kufungua kifua na kuziba tundu lililopo kwenye moyo. Taasisi hizo hivi sasa ziko katika kambi maalum ya siku sita ya upasuaji kwa wagonjwa wa moyo, katika kambi hiyo wagonjwa 20 wanarajiwa kupata matibabu.

Picha na Anna Nkinda – JKCI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...