KAMPUNI inayoongoza katika bidhaa za afya ya mdomo Whitedent imekabidhi magari 25 ya aina ya Suzuki Alto K10 kwa washindi kutoka mikoa mbali mbali nchini walioshiriki promosheni ya miezi mitatu iliyokuwa inasheherekea kuadhimisha miaka 25 ya biashara hiyo.

Kampeni hiyo ambayo ilizinduliwa rasmi Julai mwaka huu ilitoa nafasi kwa maelfu ya wananchi kushiriki shindano hilo kwa kukisia idadi ya pakiti za whitedent zilizomo ndani ya moja ya magari hayo ya aina ya Suzuki yaliyokuwa yakizunguka nchi nzima wakati wa promosheni. Washiriki walitakiwa kujaza fomu ya ushiriki katika kipindi hicho cha promosheni na kukisia jibu sahihi ili waweze kuingia katika droo kubwa ya kujishindia moja ya magari hayo ya Suzuki Alto 10 kabla ya mwisho wa Oktoba mwaka huu. 

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu Uendeshaji wa Chemi & Cotex Raja Swaminathan alisema, “Nina furaha leo ya kuyakabidhi magari haya kama ishara ya kusheherekea miaka 25 ya mafanikio pamoja na jamii yetu. Tofauti na mashindano mengine yoyote, kila mshindi atapokea gari lenye maili sifuri pamoja na kadi yake ya usajili, bima ya mwaka mmoja, likiwa limejazwa mafuta tenki nzima na gharama zote za kodi kulipwa. Hii haijawahi kufanyika nchini Tanzania.”

Shindano hilo lililokuwa chini ya uangalizi mkubwa na wa makini wa Bodi ya Bahati Nasibu Tanzania lilichukua miezi mitatu na kushirikisha mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani Zanzibar.

"Tulitaka kila mtu awe na nafasi ya kushiriki katika shindano hili. Bidhaa ya Whitedent ni ya kujivunia ya Tanzania kwa Watanzania ikiwa imetengenezwa na Watanzania. Safari ya promosheni ilipita sio mijini tu bali pia katika vijiji ili kuhakikisha kila mtu anapata nafasi ya kushiriki,” aliongeza Raja Swaminathan, Afisa Mkuu Uendeshaji wa Chemi & Cotex.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya wana Afrika mashariki milioni 14 huanza siku yao kwa kupiga mswaki kwa kutumia Whitedent. Nchini Tanzania kupitia ukaguzi wa Nielsen wa mwaka 2012 ulionyesha kuwa Whitedent ina asilimia 79 ya soko nchini na hupatikana katika maduka makubwa ya bidhaa hadi kwenye vioski vidogo. 

Whitedent, inajivunia kuwa na asili ya Tanzania na ni bidhaa inayotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu katika kiwanda chenye vifaa vya kisasa jijini Dar es Salaam. Vilevile dawa hii ya meno hutengenezwa kwa viwango vya kimataifa.

“Mafanikio makubwa ya Whitedent yanaonyesha kuwa uwezo wa viwanda nchini kwetu ni mkubwa na tuna nafasi kubwa ya kukua na kutengeneza bidhaa bora kwa Watanzania kwa bei nafuu na pia kuweza kuuza ulimwenguni kote. Tunajivunia kuwa katika viongozi wa mafanikio haya,”alimalizia Swaminathan. 

Hafla ya makabidhiano ya magari imefanyika leo rasmi katika mikoa ya Dar es Salaam, Moshi, Mbeya na Mwanza. Miongoni mwa washindi hao kutoka Dar es Salaam ni Emmanuel Sitta, Hamisi Saidi Shabani, Abdu Idd Fereshi, na Ramadhan Khamis Ramadhan. Washindi kutoka Mtwara, Arusha, Dodoma, Iringa na Shinyanga wanatarajia kupata magari yao tarehe 26 Novemba na wale kutoka Kigoma, Tabora, Morogoro, Musoma na Zanzibar tarehe 29 Novemba 2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...