Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limeyakumbusha makampuni ya simu za mkononi  hapa nchini kukamilisha taratibu za kisheria za masoko ya mitaji na hisa kwa kutoa asilimia 25 katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) ili kuwawezesha wananchi kununua hisa hizo na kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng’i Issa Kutolewa kwa hisa hizo kutawasaidia watanzania wengi kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni hizo na  pia kunufaika na gawio la kila mwaka.
“Tarehe 23 Juni, 2016, Bunge lilipitisha mswada wa sheria ya Fedha ya 2016 yaani the Finance Act 2016 pamoja na mambo mengine ulifanyia mabadiliko Sheria ya electroniki na mawasiliano  ya posta,” alisema na kuongeza kuwa ambapo makapuni ya mawasiliano yaliyoandikishwa kufanyabiashara hapa nchini kumilikisha asilimia 25 ya hisa zake kwa umma kwa kujiunga na soko la hisa la Dar es Salaam  ndani ya kipindi cha miezi sita.
Alisema zaidi ya watanzania milioni 20 wanamiliki na kutumia simu za mikono katika shughuli zao za kila siku na hivyo basi, wakati umefika kwao kama wateja wa muda mrefu kuanza kunufaika kama sehemu ya  wamiliki wa kampuni hizo kupitia hisa.
“Sisi kama baraza, nachukua fursa hii kuwahimiza watanzania wote kujiandaa kushiriki kikamilifu katika kununua hisa za makampuni hayo ya simu mara yatakapokamilisha taratibu za kujiunga na soko la hisa la DSE,”Bi. Issa alisisitiza.
Kwa mujibu wa Katibu Mtendaji huyo, Baraza litatoa elimu kwa umma kwa muda wa mwezi mmoja kupitia vyombo mbalimbali vya habari katika kuelimisha na kuhamasisha  umma kuhusu fursa hiyo muhimu kiuchumi.
“Tunapenda pia kutoa rai kwa mashirika ya Hifadhi ya Jamii nchini kuandaa utaratibu mzuri utakaowawezesha wanachama wao kuweza kushiriki katika kununua hisa za makapuni hayo ya simu mara yatakapojiunga na soko la hisa,” alisema.
Aidha, Bi. Issa alisema, Baraza linafuatilia kwa karibu sana maendeleo ya utekelezaji wa mabadiliko hayo ya kisheria na kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kwa wakati kama ilivyoainishwa kati sheria ya mwaka 2016.
 Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi lipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na linasimamia Mkakati wa Kitaifa wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kupitia madawati ya uwezeshaji kuanzia ngazi ya Wizara,Idara, Taasisi, Mikoa na Halmashauri zote nchini.
KATIBU Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’I Issa akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana wakati akiyakumbusha makampuni ya simu za mkononi  hapa nchini kukamilisha taratibu za kisheria za masoko ya mitaji na hisa kwa kutoa asilimia 25 katika soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) ili kuwawezesha wananchi kununua hisa hizo na kuwa sehemu ya wamiliki wa kampuni. Kushoto ni Ofisa Mwandamizi wa Baraza hilo, Bw. Edward Kessy.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...