Picha na – OMPR – ZNZ.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliitahadharisha Jamii kuelewa kwamba maendeleo kwa wana Taaluma wa Fani ya Sayansi iwe Maskulini au vyuoni yataendelea kuwa ndoto iwapo hakutakuwa na mipango imara ya kuimarisha miundombinu kwenye Majengo ya Maabara katika maeneo husika.
Alisema Wazazi kwa kushirikiana na Kamati za Maskuli na vyuo kupitia usimamizi wa Wizara inayosimamia masuala ya Elimu bado wana jukumu la kuhakikisha vilio vya Wanafunzi kutokana na kukabiliwa na ukosefu wa Maabara kwenye Taasisi zao vinamalizika.
Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda alitoa tahadhari hiyo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi pamoja na kulizindua rasmi Jengo la Maabara ya Skuli ya Sekondari ya Kitope iliyomo ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B”.
Jengo hilo aliloligharamia yeye pamoja na kupata msaada wa nguvu za ufadhili wa baadhi ya vifaa kutoka Ubalozi wa Jamuhuri ya Watu wa China na Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Tigo limegharimu jumla ya shilingi za Kitanzania Milioni 38,780,000/-.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe kuashiria kuzindua pamoja na kukabidhi Jengo la Maabara la Skuli ya Sekondari ya Kitope aliloligharamia yeye pamoja na ufadhili wa Ubalozi China Nchini Tanzania na Kampuni ya simu za mkononi yaTigo.
Mwalimu wa Masomo ya Sayansi wa skuli ya Sekondari Kitope Mwalimu Ali Mohamed aliyeshika kifaa cha Maabara akimuelezea Balozi Seif urahisi wa kazi yao ya ufundishaji kwa sasa baada ya kupata Maabara yenye kukidhi kiwango kinachokubalika kwa skuli za Sekondari.
Mwalimu Ali Mohamed akiendelea kutoa maelezo kwa Balozi Seif jinsi wanafunzi wa masomo ya sayansi katika skuli yao walivyofarajika kutokana na kujengewa maabara iliyokamilika kwa kazi zao za vitendo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...