Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika kulinda na kutetea haki za binadamu kwa kuzingatia maazimio mbalimbali ya ndani ya nchi na ya kimataifa ikiwemo haki ya kuishi.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo jijini Arusha kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati anafungua mkutano wa mazungumzo wa masuala ya demokrasia na haki za binadamu ya Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za binadamu.

 Amesema Tanzania ni mfano wa kuigwa barani Afrika kwa kuzingatia na kutekeleza ipasavyo mikataba mbalimbali ya kimataifa inayolenga kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma bora na za msingi ikiwemo huduma ya afya na elimu bila kubaguliwa kutokana na ulemavu,jinsia,rangi au dini.Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza na kuzingatia matamko mbalimbali ya Dunia yanayolenga kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii ikiwemo haki ya kuishi.


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameonyesha kufurahishwa na hatua zinazochukuliwa na baadhi ya nchi za Afrika katika kulinda na kutetea haki za binadamu hasa haki za wanawake na kusema kuwa bado kuna umuhimu mkubwa kwa nchi ambazo zinazosuasua kutekeleza mikataba hiyo kufanya hivyo ili kuhakikisha wanawake na watoto wanapata haki sawa katika jamii.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongozana na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati wa kuelekea kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaojadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru, mjini Arusha.
 Rais wa Mahakama ya Afrika Mhe. Jaji Justice Sylvain Ore akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.
 Wajumbe wakifuatilia kwa makini Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.

Wajumbe wakipewa jarida la Mahakama ya Afrika mara baada ya kuzinduliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara  baada kuhutubia Mkutano wa Tano wa kila Mwaka wa Ngazi ya juu wa Makama ya Afrika unaoendelea kujadili kuhusu masuala ya Haki za binadamu, demokrasia na Utawala katika bara la Afrika uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru mjini Arusha.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...