Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Abdallah Abas Kilima, ambaye pia ni mwanakamati wa kamati ya Kuzuia na Kupambana na Biashara haramu ya Kusafirisha Binadamu nchini akitoa maelezo kwa wageni kutoka Malawi namna Tanzania inavyopambana na changamoto zinazotokana na kupinga na kuzia biashara haramu ya binadamu . Wageni hao kutoka Malawi walitembelea ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa lengo la kujifunza hatua mbalimbali zinazochukuliwa nchini na wadau ili kupambana na biashara hiyo haramu. 
Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi , Seperatus Fella akizungumza wakati wa kikao na wageni (hawako pichani) kutoka nchini Malawi chini ya Kanisa la Misaada la Norway waliokuja kujifunza hapa nchini ni namna gani Taifa na wadau mbalimbali wanapambana na biashara haramu ya kusafirisha binadamu pamoja na Mpango kazi wa mwaka ili kufikia malengo. Wa kwanza ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Abdallah Abas Kilima, ambaye pia ni mwanakamati wa kamati ya Kuzuia na Kupambana na Biashara haramu ya Kusafirisha Binadamu. 
Mkuu wa Programu wa Kanisa la Misaada la Norway nchini Malawi Bi. Hayley Elizabeth Webster (katikati) akiuliza swali kwa kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu hawapo pichani kwa namana gani serikali imejipanga kupambana na biashara hiyo kwa kutoa elimu kwa jamii licha ya kuwa na bajeti finyu kama ilivyo elezwa na mmoja wa wanakamati hao. Wengine ni wajumbe kutoka kanisa hilo la Misaada nchini Malawi walioambatana nae ili kujifunza namba ambavyo Tanzania imekua ikipambana na biashara hiyo.
Katibu wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Seperatus Fella (wa pili kulia), akizungumza wakati wa kikao na wageni kutoka nchini Malawi chini ya Kanisa la Misaada la Norway waliokuja kujifunza hapa nchini ni namna gani Taifa na wadau mbalimbali wanapambana na biashara haramu ya kusafirisha binadamu pamoja na Mpango kazi wa mwaka ili kufikia malengo. Wa kwanza ni Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati, Balozi Abdallah Abas Kilima, ambaye pia ni mwanakamati wa kamati ya Kuzuia na Kupambana na Biashara haramu ya Kusafirisha Binadamu.
Baadhi ya Wanakamati wa Kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu na wajumbe kutoka nchini Malawi chini ya Kanisa la Misaada la Norway wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza majadiliano yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi juu ya namna Tanzania inavyopambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...