Mama wa Mitindo Mkongwe anayefanya vizuri ndani ya Tanzania na Nchini Marekani, Asya Idarous Khamsini jumamosi ya Novemba 26.2016 anatarajia kuwakilisha Tanzania katika usiku maalum wa African fashion Week Boston, Marekani.
Jukwaa hilo maalum la mitindo limeandaliwa na House of Nadhra Boston USA, huku mbali na Mama wa Mitindo Asya Idarous, pia litajumuisha Madesigner kutoka kona za Afrika, Ulaya na kwingineko.
Tukio linatarajia kuwa na watu mbalimbali watakaojumuika pamoja kushuhudia mavazi ya ubunifu hasa kwa ubunifu wa hali ya juu kutoka kwa wabunifu wa Afrika. Pia mbali na jukwaa hilo la mitindo pia kutakuwa na muziki wa ‘Live band’. Vyakula maalum vya kiafrika, pamoja na uuzwaji wa bidhaa za kiafrika.
Eneo la tukio hilo: Hibernia Hall, Boston, MA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...