Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Jacob Kibona akiwaonyesha Waandishi wa Habari (hawapo pichani) Kitabu cha wageni chenye nembo ya serikali, alisema wakala wake pekee ndiyo wenye mamlaka ya kusambaza vitabu hivyo na nyaraka mbalimbali za serikali zenye nembo hiyo kwa taasisi za umma kwa lengo la kulinda uhalisia wa nembo ya serikali yenye alama ya Bibi na Bwana.

Na Barnabas Lugwisha

Serikali kupitia Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) hivi karibuni imeokoa shilling bilioni 1.3 baada ya wakala hiyo kununua kwa pamoja magari 392 katika mpango wa serikali wa manunuzi ya pamoja.

Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala hiyo, Bw Jacob Kibona, amewaambia Waandishi wa Habari jana kuwa fedha hizo zimeokolewa na serikali baada ya kununua magari 392 kwa pamoja kwa Sh. bilioni 56.1 badala ya shilingibilioni 58.1 iwapo kila taasisi ingenunua magari yake.

“Kwa kweli huu mpango wa manunuzi yapamoja ni mpango mzuri sana ambao unaiwezesha serikali kuokoa fedha nyingi,” Alisema

Alisema fedha zilizookolewa zitaiwezesha serikali kufanya shughuli nyingine za maendeleo ya ummana kama vile kuboresha miundombinu ya barabara, huduma za afya na elimu.
 
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA) Jacob Kibona akiwaonyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) faili lenye nembo ya serikali, alisema wakala wake pekee ndiyo wenye mamlaka ya kusambaza mafaili hayo kwa lengo la kulinda uhalisia wa nembo ya serikali yenye alama ya Bibi na Bwana.


Amesema taasisi yake pia katika kipindi cha Julai hadi Oktobamwaka huu, imezikabidhi taasisi za serikali magari ya aina mbalimbali yapatayo 136.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...