MAOFISA wawili wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na rushwa ya Sh milioni 25 kwa ajili ya kupanga matokeo.
Washtakiwa hao Kaimu Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Martin Chacha (picha ya juu) na Msaidizi wa Rais wa shirikisho hilo, Juma Matandika (picha ya chini), walifikishwa mahakamani hapo jana.
Walisomewa mashtaka yao na Wakili kutoka Taasaisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Leonard Swai pamoja na Wakili wa Serikali Odesa Horombe mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Wakili Horombe alidai kuwa Februari 4, mwaka huu katika ofisi za Makao Makuu ya TFF, washtakiwa hao waliomba rushwa ya Sh milioni 25 kutoka kwa Salum Kalunge na Ofisa wa Shirikisho la Soka mkoani Geita na Klabu ya Mpira wa Miguu ya Geita, Constantine Morandi.
Inadaiwa waliomba fedha hizo kwa ajili ya kuishinikiza na kuishawishi TFF na Idara ya Uhamiaji kupanga uamuzi wa matokeowa mechi ya Klabu ya Mpira wa Miguu ya Tabora ili kuisaidia klabu ya Geita Gold  iweze kupanda daraja na kucheza Ligi Kuu ya Soka Tanzania, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za mwajiri wao.
Washtakiwa walikana mashtaka na Wakili Horombe alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kumba tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza kusikilizwa, pia hana pingamizi na dhamana.

Washtakiwa hao waliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu wenye vitambulisho, waliosaini hati ya Sh milioni tano kwa kila mmoja.
Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 30, mwaka huu, kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...