Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni amewaasa abiria kutoa taarifa pale wanapoona dereva anahatarisha maisha yao katika vyombo vya usafiri.

Masauni ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Paza Sauti iliyoratibiwa na Mabalozi wa Usalama Babarani RSA Tanzania katika Kituo cha mabasi ya Mikoani na Nchi Jirani cha ubungo jijini Dar es Salaam, amesema kila mtu anawajibu wa kutoa taarifa dhidi ya dereva anayehatarisha maisha katika vyombo vya usafiri.

Amesema dereva kutojua sheria za usalama barabarani isiwe kigezo cha kuvunja sheria zilizowekwa kutokana na waathirika wa ajali ni watanzania ambao ndio nguvu kazi ya taifa.

Amesema kampeni hiyo iweze kuleta matokeo chanya ambayo yataonyesha kupungua kwa ajali au kutokuwepo kwa ajali na kufanya watanzania kuwa salama katika vyombo vya usafiri.

Nae Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP), Mohamed Mpinga amesema kampeni iliyozinduliwa ni jitihada za kikosi cha usalama barabarani katika kupambana na ajali pamoja na kuongeza askari kila sehemu ambayo dereva wamekuwa wakikiuka sheria za usalama barabarani.

Amesema abiria wanatakiwa kuwa chachu ya kutoa taarifa za uvunjifu wa sheria za usalama barabarani kwa madereva ili waweze kuchukulia hatua.

Mjumbe Usalama barabarani Mkoa Dar es Salaam, Idd Azzan amesema kampeni hiyo ni italeta mageuzi katika kupunguza ajali.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto) akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti ndani ya basi la Machame Express katika Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo iliandaliwa na Mabalozi wa RSA kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali nchini. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na abiria mara baada ya kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti katika Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka abiria nchini kutoa taarifa kwa haraka pindi wanapoona dereva anavunja sheria na pia kila abiria ni wajibu wake kujua haki zake. Kushoto ni Mlezi wa RSA Taifa ambaye pia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Naibu Kamishna, Mohamed Mpinga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia) akimsikiliza Katibu wa Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA) Taifa, Asina Omary alipokuwa anatoa historia ya RSA pamoja na majukumu yake kabla ya Naibu Waziri huyo kuzindua Kampeni ya Abiria Paza Sauti katika Kituo Kikuu cha Mabasi, Ubungo jijini Dar es Salaam leo. Kampeni hiyo iliratibiwa na Mabalozi wa RSA kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...