Baadhi ya Mashabiki wa Timu ya Mbeya city wakoma kumwanya wakishangilia ushindi wa gori 2,1 kwa kuibugiza timu ya Yanga leo katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

MABINGWA watetezi wa ligi kuu Vodacom Yanga wameshindwa kufurukuta mbele ya Mbeya City baada ya kukubali kipigo cha goli 2 - 1 dhidi ya Mbeya City mchezo uliochezwa katika uwanja wa CCM Sokoine jijini Mbeya. 

Kipindi cha kwanza kilianza kwa kasi kwa timu ya Mbeya City kupata goli dakika ya sita kupitia kwa Hassan Mwasapili ikiwa ni mpira wa adhabu uliopigwa nje ya 18 na Kenny Ally kuaindikia goli la pili ikiwa nalo ni adhabu ambalo lilileta utata baada ya mwamuzi kulikataa na kisha kulikubali. 

Kutokana na hali hiyo wachezaji wa Yanga walianza kuliandama goli la Mbeya City na katika dakika ya 45 ya kipindi cha Kwanza Donald Ngoma anaiandikia Yanga goli la kufutia machozi ambalo lilidumu mpaka kipindi cha mwisho. 
Na katika mchezo mwingine timu ya Simba imejihakikishia kuendelea kukaa kileleni baada ya kuoata ushindi wa goli 1­0 dhidi ya Stand United baada ya mshambuliaji wao Shiza Kichuya kuiandikia timu hiyo goli la uushindi kwa mkwaju wa penati. baada ya matokeo hayo Simba imeendelea kujikita kileleni kwa alama 35 nyuma ya alama 27 za mabingwa watetezi Yanga. 
Mchezaji wa Yanga  Kelvin Yondani jezi Nambari 5 mgongoni akibishana  muamuzi katika Mtanange wa Mbeya city na yanga Uwanjani Sokoine Jijini Mbeya..
  
Tuambieee Hilo ni Goliiii au sio Goliii....
PICHA ZOTE NA MR.PENGO MMG MBEYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mbona kila mechi jezi ya Yanga ni manjano tofauti????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...