Kama ilivyoripotiwa hapo awali, Shiikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) baada ya kutoridhika na kujiridhisha kuwa mmoja wa wachezaji wa Jamhuri ya Congo-Brazzaville, alikiuka kanuni za mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17, mwaka huu  lilimkatia rufaa mchezaji Langa-Lesse Bercy katika Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
Kutokana na rufaa hiyo dhidi ya mchezaji huyo wa Congo, Langa Lesse Bercy, CAF liliagiza apelekwe Makao Makuu ya Shirikisho hilo, lililoko Cairo, Misri  kwa ajili ya kurudia na kuthibitisha umri wake kwa kipimo cha MRI (Magnetic Imaging Resonance).
TFF iliagizwa na CAF igharimie zoezi zima ikiwa ni pamoja na kulipia gharama za usafiri wa mchezaji husika na daktari wake  pamoja na kulipia gharama za vipimo. TFF ilikubaliana na matakwa hayo ya CAF na kulipia.
Kipimo ilikuwa kifanyike leo Novemba 19, 2016 saa 5.00 asubuhi mjini Cairo, Misri. Ujumbe wa TFF wa watu wanne ukiambatana na madaktari wawili uliwasili mjini Cairo tangu Novemba 17, 2016 ili  kuwa shuhuda wa zoezi la kipimo hicho.
Jana usiku saa 5.00 TFF ilipokea ujumbe kutoka CAF kuwa mchezaji Langa Bercy ameshindwa kusafiri kwenda Cairo kwa kuwa yuko katika eneo lililoko "vitani",eneo hilo halikutajwa.
TFF inaendelea kufuatia kwa karibu jambo hili ili kuhakikisha haki inatendeka .
Kadhalika Aidha TFF inaomba wadau wa mpira wa miguu wawe na subira katika kipindi hiki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...