Na Nteghenjwa
Hosseah - Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amewataka wafadhili na wadau wa watoto
kubuni miradi inayoendana na kusaidia
Mpango wa Serikali wa Elimu bure kwa shule za Msingi na Sekondari ili kupunguza changamoto zinazojitokeza kwa
sasa na kuuwezesha mpango huu kutekelezwa kwa mafanikio makubwa.
Mhe. Gambo ameyasema
hayo wakati wa Mkutano wa kushirikishana tuliojifunza wakati wa utekelezaji wa
mpango wa pamoja tuwalee uliotekelezwa kwa miaka sita kwenye Kanda ya
Kaskazini na ambao kwa sasa umemaliza
muda wake ulifanyika kwenye Hotel ya Mt Meru Jijini hapa.
Akizungumza katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa
amesema kazi kubwa imefanyika wakati utekelezaji wote wa mradi na mafanikio yake tumeonekana kwani watoto wamefikiwa
na kusaidiwa kutoka katika mazingira hatarishi yaliyokuwa yanawakabili na
wengine kupatiwa kadi za msamaha wa matibabu na zaidi mradi huu umekabidhiwa
kwa Halmashauri husika ambazo
zitaendelea kusimamia na kutekeleza
mipango iliyowekwa chini ya mradi wa Pamoja Tuwalee.
Aliendelea kusema kuwa kukamilika kwa mradi
huu katika awamu ya kwanza ni wazi kabisa kwamba ni maandalizi ya mradi
mwingine ambao utakua na malengo yanayoshabihiana na programu ya awali hivyo ni
vyema kwa kuwa walengwa bado ni watoto niwatake wadau kubuni miradi utakaolenga
kusaidia Elimu bure na kwa kuwa watoto wote wanapata Elimu bure kupitia mpango
huu basi ni vyema mkaelekeza nguvu kwenye utoaji wa Chakula kwa wananfunzi
suala ambalo tumeona ni changamoto kwa watoto wetu.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha akizungumza na wadau wa Mkutano
Mkurugenzi wa WEI-TANZANIA Bi. Lilian Badi (aliyesimama) akielezea mafanikio ya Mradi wakati wa Mkutano wa kuhitimisha mradi wa Pamoja Tuwalee.
Mkurugenzi Mkuu wa World Education Inc Bi.Gill Garb akitoa taaria ya utekelezaji wa mradi wa Pamoja Tuwalee kupitia WEI-Bantwana.
Mwakilishi wa US-AID Tanzania Bi. Maria Busquets akielezea namna ambavyo Shirika lake limefanikisha utekelezaji wa mradi wa Pamoja Tuwalee.
Mkurugenzi wa Kituo cha Maendeleo ya Wanawake, watoto na vijana (CWCD) Bi. Hindu Ally Mbwego akielezea mafanikio ya mradi kupitia Kituo chake ambao ndio watekelezaji katika Halmashauri za Jiji la Arusha, Karatu na Moshi.
Picha ya pamoja ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha (katikati mbele), Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi waliotekeleza mradi huu, viongozi wa WEI, US AID, CWCD pamoja na Wadau wa watoto walioshirki katika Mkutano wa kuhitimisha mradi wa Pamoja Tuwalee.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...