Tembo wa Asia
Na Pamela Mollel,Mikumi

Tembo ni mnyama kubwa kuliko wote lakini sio mrefu kama twiga,kuna aina mbili ya tembo.tembo w a bara la Afrika na  bara la Asia 

Ukitaka kujua tofauti zao wa bara la Afrika ni wakubwa ,na maskio yao yanamuonekano wa ramani ya bara la afrika lakini tembo bara la Asia wanamasikio madogo na pia wanaweza kufundishwa kulima na michezo mbalimbali

 Akizungumza na waandishi wa habri kuhusu mnyama huyo (Tembo)Afisa wa shirika la Tanapa katika hifadhi ya Mikumi Abdalla Choma alisema kuwa Tembo hao wa  wa bara la Afrika wapo katika makundi mawili,1.      Tembo wa msituni wanameno ambayo  yamenyooka kwaajili ya kuwawezesha kupita katika msitu
2.       Tembo wa Savana, meno yao yamepindapinda wanapenda kuishi katika familia moja wanaweza kuishi kwanzia wawili hadi 45 kwa familia
Alisema Tembo wauwezo mkubwa wa kusikia na wanakumbukumbu ya kutosha
Akizungumzia kuhusu uzazi wa tembo mzee Chuma alisema kuwa tembo wanauwezo wa kubeba mimba na kuzaa kwa miezi 18-20
 
Tembo wa bara la Afrika
Tembo huyo hunyonyesha motto wake kwa takribani miaka miwili hadi mitatu na motto wa tembo huyo akishafikisha miaka 15 huesabika ameshakuwa na kutakiwa kuondoka katika familia hiyo na kwenda kujitegemea
Tembo huishi kwa miaka 60-75 kwa sasa lakini miaka ya nyumba walikuwa na uwezo wa kuishi miaka 80-120 .“Sababu za kuishi miaka michache kwa miaka hii ni kutokana na mabadiliko ya tabia nchi “alisema mzee Mchoma
CHAKULA CHA TEMBO
Hupendelea kula matawi ya miti na nyasi za chini,pia hupenda kula kwa masaa 16 kati ya masaa 24,Kiasi cha chakula anachokula ni kati ya 150-300 kg kwa tembo mkubwa na hunywa maji kati ya lita 200 hadi 250

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...