Na Daniel Mwambene, Songwe                           

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje wampongeza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Haji Mnasi kwa kukuza uchumi wa wilaya hiyo na kufanikiwa kuwadhibiti wafanyabiashara waliokuwa wakikwepa kodi.
Pongezi hizo zilitolewa na madiwani hivi karibuni wakati wa kikao cha Kamati ya Fedha,Uongozi na Mipango kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri.
Akizungumza na blog hii diwani wa kata ya Itumba Mohamed Mwala alisema kuwa wanatambua juhudi zilizofanywa na Mkurugenzi Haj Mnasi na wafanyakazi wa halmashauri kukusanya ushuru maeneo mbalimbali na kufanikiwa kuyakamata magari aina ya maroli yaliyokuwa yakikwepa ushuru.
Naye diwani wa kata ya Ibaba Tata Kibona alisema kuwa mkurugenzi na timu yake  wamekuwa wakitembea usiku kuwatafuta wakwepa kodi hasa kwenye kata yake ambapo mara kadhaa mkurugenzi huyo amekuwa akionekana nyakati za usiku.
"mimi sijawahi ona mkurugenzi kama huyu maana anaacha usingizi wake unamkuta kwenye kata nyakati za usiku akipambana nao wakwepa kodi na amefanikiwa kuwadhibiti wafanyabiashara wote wakwepa kodi na ndio maana sasa mapato yameanza kukua kwa kasi katika wilaya yetu"alisema Kibona 
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ileje Haji Mnasi akiwa kwenye eneo husika la kukagua wakwepa kodi.
 
Hawa ni baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wialaya ya Ileje wakifutalia jambo lililokuwa likiongelewa na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya ileje haji mnasi
Hili ni moja ya malori yaliyokuwa yakikwepa ushuru kwa kufanya biashara ya kushusha mizigo vichochoroni.
Hili ni moja kati ya gari linalobeba milunda bila kulipia ushuru na mkurugenzi Haji Mnasi kufanikiwa kulikamata wakati wa zoezi maalumu la kuwatafuta wakwepa kodi waliobobea kuikimbia serikali kulipa kodi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...