Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela amezindua mradi wa maji katika kijiji cha Lupalama kilichopo katika Tarafa ya kalenga Wilayani Iringa uliodhaminiwa na  Shirika la E.P.I.C (Everyday People Initiate Changes) la Marekani liloanzishwa na Mwanamuziki wa Marekani Tinara Moore. ambaye aliwahi kutembelea Tanzania na baadae kuamua kutoa misaada mbalimbali. 
Wanakijiji wa Lupalama kwa muda mrefu wamekuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji, “Tulikuwa tukilazimika kutembea saa zima kufata maji mtoni nabado maji haya kuwa ya uhakika kwa maana kipindi cha kiangazi mto ulikuwa una kauka jambo lililopelekea kupata shida kubwa sana katika upatikanaji wa maji”  anaeleza Bi Theobadina Ngailo mkazi wa Lupalama anaongeza kuwa “Tulikuwa tunatumia hata maji ya kwenye vidimbwi ambayo sio salama kwa matumizi ya binadamu kwani muda mungine tulikuwa tukichangia maji hayo na mifugo jambo lilipolekea kulipuka kwa magonjwa kama kuhara”. 
Akizungumza wakati wa kukabidhi mradi huo Muwakilishi wa E.P.I.C Tanzania Bwana Johnson Mkini Kisinda amsema kuwa mradi huo umeghalimu pesa zaidi ya milioni therasini na tano hadi kukamilika “Hiki ni kisima cha pili kwa urefu katika visima vyote tulivyo chimba kwani Lengo lilikuwa kuchimba mita sabini tu ila tulikosa maji tukalazimika kuchimba mita mia moja na themanini kwenda chini hadi kuyafikia maji”, pia ame waasa wanakijiji wa Lupalama kuwa walinzi wa miundo mbinu hiyo ya maji kwani ni kwa faida yao wenyewe. 
Akikabidhi Mradi huo kwa wanakijiji wa lupalama mkuu wa wilaya ya Iringa amewaomba  wana kijiji hao kuusimamia vema mradi huo kwani Ofisi yake ina mpango wa kuhakikisha maji hayo yana sambazwa katika Maeneo Yote ya kijiji hicho ili kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa wingi “Ni ndoto yangu kuona Maji haya yana wafikia wanakijiji wote wa lupalama ikibidi na maeneo ya Jirani wapate pia maji haya nitoe agizo kwa serikali ya kijiji kuunda kamati ya kusimamia na kutunza mradi huu ili uendelee kufanya kazi na kunufaisha wengi wakati mimi niki hangaika kuona jinsi gani tunapata pampu ya Umeme ikishindikana hata ya kutumia nguvu ya jua ili tusambaze maji haya sehemu nyingi zaidi”. 
Pia ameagiza Serikali ya kijiji Kuanza mara moja Mchakato wa ujenzi wa kituo cha afya kijijini hapo kwani ni kero ya muda mrefu hasa kwa akina mama kwani wana lazimika kutembea kilomita saba kufuata huduma ya afya “Nawaombeni Zoezi hili  lianze mapema sana na ikibidi kila mwanakijiji ashiriki kukusanya mawe ya ujenzi na pindi mkiwa tayali ujenzi uanze mara moja”. 
Katika hotuba yake Mkuu wa wilaya pia amehimiza watu kutunza chakula “ mvua mwaka huu sio za kuridhisha hivyo basi ipo hofu ya kukosekana chakula ni muhimu wananchi wakatunza chakula na kulima mazao yenye kuhimili ukame”
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akikata utepe kuzindua mradi wa maji katika kijiji cha Lupalama kilichopo katika Tarafa ya Kalenga Wilayani Iringa. Kulia kwake ni bwana Johnson Kisinda muwakilishi wa E.P.I.C Tanzania Kushoto ni Diwania wa Lupalama.
  Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akichota maji baada ya  kuzindua mradi  huo katika kijiji cha Lupalama kilichopo katika Tarafa ya Kalenga Wilayani Iringa
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela akimtiwka Bi. Theobadina Sengailo ndoo ya maji baada ya  kuzindua mradi  huo katika kijiji cha Lupalama kilichopo katika Tarafa ya Kalenga Wilayani Iringa
 Wananchi wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh Richard Kasesela katika hafla ya  kuzindua mradi wa maji  katika kijiji cha Lupalama kilichopo katika Tarafa ya Kalenga Wilayani Iringa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...