Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Fadhili Nkurlu amezindua kifaa cha kubaini moto ukiwa katika hatua ya moshi (smoke detector) wilayani humo. Tukio hili limefanyika katika shule ya sekondari Dakama ambapo Mhe. Nkurlu amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote tatu za wilaya ya Kahama kuhakikisha kwamba kifaa hicho kinafungwa kwenye shule na mabweni yote ili kutekeleza agizo la serikali la kupambana na moto mashuleni.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Dakama wakijifunza namna ya kutumia kifaa cha kubaini moto ukiwa katika hatua ya moshi (smoke detector)
Wanafunzi wa shule ya sekondari Dakama wakioneshwa namna ya kifaa cha kubaini moto ukiwa katika hatua ya moshi (smoke detector) kinavyofanya kazi
Wanafunzi wa shule ya sekondari Dakama wakiwasha moto kukijaribu kifaa cha kubaini moto ukiwa katika hatua ya moshi (smoke detector)
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Fadhili Nkurlu akiwa na Wanafunzi wa shule ya sekondari Dakama wakati wa kujifunza namna ya kutumia kifaa cha kubaini moto ukiwa katika hatua ya moshi (smoke detector)
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Fadhili Nkurlu akielekeza wanafunzi wa shule ya sekondari Dakama wakati wa kujifunza namna ya kutumia kifaa cha kubaini moto ukiwa katika hatua ya moshi (smoke detector)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...