Na Saimeni Mgalula,Songwe
WAFANYA BIASHARA katika Mji wa Tunduma uliopo wilaya ya Momba mkoani hapa wamemueleza mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Juma Irando juu ya changamoto  zilijitokeza baada ya wadau hao wa maendeleo ya kijamii na vikundi mbalimbali vya kijamiii kukutana naye kwa  lengo la kusikiliza changamoto zinazowakabili pamoja na kujadili nao juu ya ushirikishwaji wao katika utatuzi wa changamoto hizo.
Changamoto waliyoitaja ni maji  na upatikanaji wake. Walisema mji wa Tunduma hauna mfumo wa upatikanaji wa maji hivyo hulazimika kutegemia maji ya visima. Walitaja pia suala la kodi ya mapato wanazotozwa wakipeleka lawama zao kwa maofisa wa ukusanyaji wa mapato.
Pia wamiliki wa mahoteli na nyumba za kulala wageni walilalamikia suala la ukaguzi wa wateja wao linalofanywa mara kwa mara na vyombo vya ulinzi na usalama, Walisema hoteli moja inaweza kukaguliwa mara tano na vyombo vya ulinzi tofauti  na kuonekana kuwa ni usumbufu kwa wateja.
''Pia wafanyabiashara tunanyanyaswa kwa kukamatwa kwa biashara zinazovushwa mpakani mwa Tanzania na Zambia upande wa tanzania wakati wenzetu wa upande wa zambia huachiwa'', walisema
 MKurugenzi wa halmashauri ya mjiwa Tunduma Bw. Valery Kwembe aliwaambia wafanya biashara hao kuwa suala la maji linafanyiwa kazi na tayari kuna mradi wa maji umeanza kutekelezwa ambao utakuwa ni suhilisho kwa wakazi wa Tunduma.
Pia mkuu wa kituo cha polisi cha tunduma OCS Kakoti aliwatoa hofu wafanyabiashara hao kuwa kwa wale wanaofuata sheria na taratibu huwa hawakamatwi lakini kwa wasio fuata sheria huchukulia hatua na kupewa maelekezo.
''Wafanya biashara naombeni kila mmoja anapovuka katika mpaka huo kuhakikisha kuwa wanakuwa na risiti halali za mizigo pindi wanapovuka mpaka au kusafirisha bidhaa zao''alisema OCS Kakoti.
Mkuu  wa wilaya Mhe Juma Irando alimalizia kwa kusema kuwa changamoto hizo ameshazipata na atahakikisha kuwa anazifanyia kazi kwa wakati. 
"Hii ni  kuhakikisha kuwa hakuna ambae anaonewa ili tuweza kuwa wamoja katika suala la kuhakikisha kuwa amani inakuwepo katika mji wetu kama hivi sasa.
''Naomba wafanya biashara na watu wengine kuhakikisha kuwa tunashikamana kwa kuleta maendeleo katika wilaya yetu ili iweze kusonga mbele hasa na sio kwa kutumia nguvu. Tunafanya kama hivi leo panapo kuwa na tatizo'', alisema DC.
  Wafanyabiashara katika Mji wa Tunduma katika mkutano na Mkuu  wa wilaya ya Tunduma Mhe Juma Irando na viongozi wengine wa wilaya

Mkuu  wa wilaya ya Tunduma Mhe Juma Irando akiongea katika mkutano huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...