Evelyn Mkokoi na Anceth Nyahore Kahama

SIKU moja baada ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano
Mazingira Luhaga Mpina,kubaini ukiukwaji mkubwa wa usimamizi wa sheria za Mazingira na Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC)kuiadhibu kulipa faini ya shilingi milioni 15,jana Naibu Waziri huyo amebaini umwagaji wa maji taka ovyo katika dampo la tala la Busoka mjini hapa.

Naibu waziri huyo katika ziara yake ya siku ya pili yenye staili ya
kushitukiza na kuachana na ratiba aliyopangiwa, alishuhudia uchafuzi
wa mazigira wa gari moja aina la Fuso lenye namba za usajili T 245 BHC
linalomilikiwa na Shule ya Msingi ya Kwema ya mjini Kahama lililokuwa
likiendeshwa na Johanas Mwambeya,likimwaga maji taka kando ya barabra
karibu na dampo hilo.

Naibu Waziri huyo, aliyekuwa amefauatana na Wakaguzi wa Mratibu wa
NEMC kanda ya Ziwa,Jamal Baruti, alisema kitendo hicho ni hujuma
katika mazingira na ukiukwaji wa kifungu namba 187 cha utunzaji wa
mazingira na kuagiza halmashauri hiyo ndani ya siku saba iwe imechimba
bwawa maalum kwa ajili ya kumwaga maji taka na kutoa adhabu ya mmliki
wa gari hilo kulipa shilingi milioni 1.2 ambazo mmiliki huyo alilipa
mara moja..

“Ni jana tu adhabu ya shilingi milioni 15 imetolewa kwa halmashauri ya mji wa Kahama kwa ukiukwaji wa usimamizi wa sheria za utunzaji mazingira, na leo tunashuhudia uchafuzi mkubwa,tumepita maeneo mengi hatujaona
hali hii ya umwagaji vinyesi tena kando ya barabara na ni mchana
kweupe….umwagaji katika eneo hilo la tambalare kuelekea katika vyanzo
vya maji inasikitisha kweli kweli”Alisema Mpina.
 Gari la Kuzolea majitaka no T245 BHC mali ya shule ya kwema ya mjini Kahama lililokamatwa likimwaga maji taka  katika eneo la barabarani lisilo rasmi leo ambapo Dereva wa gari hilo Bwana Thomas Mwambeya pamoja na kutozwa faini ya shi milioni 1.2 likamatwa na kufishwa katika kituo cha police cha Mjini Kahama.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina katika Ziara ya kukagua DAMPO la Majitaka Mjini Kahama akionyesha namna ambavyo maji taka yanayomwagwa kiholela yalivyoenea kwa wingi katika eneo  la karibu na barabara.
Naibu Waziri Ofisi ya Makmu wa Rais Muungano na Mazingira (katikati katika Ziara ya Mgodi wa Dhahabu wa Bulyankulu Wilayani Kahama. (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...