KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, inatarajia kuendelea na mpango wake wa kitaifa wa kusaka wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 (U-17) Jumamosi Ijayo Novemba 19, mwaka huu (kesho) katika Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya kuanzia saa 1.00 asubuhi hadi saa 8.00 mchana.

Azam FC wikiendi iliyopita iliendesha zoezi hilo Dar es Salaam lililohudhuriwa na vijana 433 na kuchaguliwa saba pekee, na hivyo kufanya idadi kamili ya waliochaguliwa kwenye mchujo wa kwanza kufikia 50 miongoni mwa vijana 2,593 walisailiwa mpaka sasa katika maeneo manne ambayo Azam FC imeendesha zoezi hilo (Dar es Salaam, Tanga, Morogoro & Dodoma na Visiwani Zanzibar).

Mara baada ya zoezi hilo kukamilika kwenye maeneo yote, vijana wote watafanyiwa mchujo wa mwisho mwezi ujao katika Uwanja wa Azam Complex kabla ya timu hiyo kuundwa rasmi kwa vijana bora watakaofanya vizuri kuchukuliwa.

Vijana wanaotakiwa kuhudhiriwa zoezi hilo na wale walizaliwa kuanzia mwaka 2000, 2001, 2002, 2003 au 2004, ambapo uhakiki wa vyeti utafanyika kwa wale watakaochaguliwa.

Kwa majaribio mengine ya wazi katika maeneo mengine kuzunguka Tanzania yatatangazwa hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...