Na Theresia Mwami TEMESA Katavi.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amemuagiza Meneja wa TEMESA Katavi Mhandisi Sunday Kyungai kuwatumia wataalamu waliohitimu katika chuo cha VETA kilichoko Mpanda ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa mafundi katika kituo hicho.

Dk Mgwatu ametoa agizo hilo alipotembelea Kituo cha TEMESA Mkoani Katavi na kujione utendaji kazi wa kituo hicho.“Nakuagiza Meneja katika kuajiri wataalamu mzingatie wataalam hasa wale waliohitimu kutoka Vyuo vya VETA nchini” alisisitiza Dk Mgwatu.

Dkt Mgwatu ameongeza kuwa vituo vya wakala huyo vinatakiwa kuwa wabunifu katika kutatua matatizo mbalimbali badala ya kutegemea kila kitu kutoka Makao Makuu ya TEMESA.Aidha Dkt. Mgwatu amemuagiza Mhandisi Kyungai kuwasilisha kwake mpango wa kujenga karakana mpya kwenye eneo jipya la TEMESA lililopo Katavi katika mji wa Mpanda.

Kwa upande wake Meneja wa TEMESA Katavi Mhandisi Sunday Kyungai amemuhakikishia Mtendaji Mkuu kuwa watazingatia kuajiri watumishi wa TEMESA katika kituo cha Katavi kwa kuzingatia agizo alilolitoa la kupata wataalamu kutoka vyuo vya VETA nchini.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yuko katika ziara ya kikazi katika vituo vya TEMESA Nyanda za Juu Kusini kutembelea na kukagua vituo hivyo ili kujionea changamoto mbalimbali pamoja na utendaji kazi wake.
 
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kulia) akizungumza na Meneja wa TEMESA Katavi Mhandisi Sunday Kyungai (kushoto), alipotembelea kituoni hapo.Picha na Theresia Mwami TEMESA Katavi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...