Na Amina Kibwana,Glabu ya Jamii
Muungano wa wapiga
kura Tanzania (TANVU) umeandaa matembezi ya Hiayari ya upandaji mti kwa
lengo la kuunga mkono Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya
Awamu ya tano.
Matembezi hayo yanatarajiwa
kuanza rasmi Novemba 26 hadi 30,2016, ambayo yataanzia Mkoani
Singida wilaya ya Ikungi hadi Mkoa wa Dodoma ambapo zaidi ya wazalendo 600
wnatarajiwa kuhudhuria katika matembezi hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mratibu Msaidizi na Katibu
mwenezi,Habari na Mawasiliano Barrynice Mayunga amesema kuwa katika
matembezi hayo kutakuwa na upandaji wa miti ipatayo 12,500 (Elfu kumi
na mbili na miatano) kwa ajili ya utunzaji wa mazingira na misingi
endelevu kwa viwanda.
Amesema Mayunga, kwa
kufanya hivyo pia itasaidia kujenga na kudumisha uzalendo ndani ya mioyo
ya watanzania pamoja na kufanya kazi kwa kutumia kauli mbiu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli wa Hapa kazi tu.
"Sisi kama
wazalendo tumeamua kujitoa kwa kufanya mate mbezi ya hiyari ili tuweze
kukamilisha shughuli za upandaji miti kwa kuisaidia serikali ya awamu ya
tano katika kuzisimamia rasilimali za nchi yetu."
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango na Uwezeshaji John Meena amesema
kuwa miti ni pamoja na mikakati ya utunzaji wa mazingira kwani bila kuwa
na miti kunaweza kusababisha madhara mbalimbali katika nchi ikiwemo,
kuharibika kwa mifugo, kusababisha ukame nchini, Kupotea kwa mazao ya
asili kama mbao,asali na matunda pamoja na kushuka kwa uzalishaji wa
mazao na kuharibika kwa miundombinu ya hali ya hewa.
Hata hivyo Muungano wa wapiga kura Tanzania (TANVU) umetoa wito kwa
wanachi wote kujiandikisha na kuungana nao katika matembezi haya ili
waweze kufikia lengo kwa pamoja kama wazalendo, Pia wameipomgeza
serikali yaawamu ya tano kwa jitihada inayoionesha katika kusimamia
masuala mazima ya uwajibikaji kwa wanachi wake.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...