Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeimarisha nafasi yake ya kutoa huduma za afya kama hospitali ya taifa ili kupunguza rufaa za wagonjwa wanaokwenda nje ya nchi kutibiwa.

Muhimbili imejipanga kutoa huduma katika ubora wa hali ya juu na tayari imepeleka wataalamu wake nje ya nchi ili kujengewa uwezo wa kutoa huduma kwa wagonjwa.

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Buberwa Aligaesha amesema Muhimbili imepeleka wataalamu 20 nchini India kwa ajili kujifunza upandikizaji figo pamoja na kutoa huduma bora kwa wagonjwa wenye matatizo ya figo.

Aligaesha amesema madaktari na wataalamu wengine wamerejea kutoka India ambako walikwenda kujifunza upandikizaji wa vifaa kwa wagonjwa wenye matatizo ya masikio.
 Jengo la Kinamama ‘Maternity Block Two’ ambalo Rais John Magufuli aliagiza litumike kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa. Jengo hilo sasa linalaza wagonjwa 90. Awali jengo hilo lilitumika kama ofisi.
 Huduma za vipimo vya radiolojia zimeimarika na kusababisha wagonjwa wengi kupatiwa huduma za vipimo kwa wakati.
 Pichani ni wodi 18 imekarabatiwa kwa ajili ya wagonjwa binafsi.
Sehemu ya mapokezi idara ya dharura.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...