·
Nacte yafuta leseni ya vyuo vya ufundi
26
·
20 vyasimamishiwa programu zisizosajiliwa na baraza hilo
·
2 vyasimamishwa kwa kutokuwa na usajili
Baraza
la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifungia vyuo vya ufundi 26
kutokana na makosa mbalimbali, ikiwamo kushindwa kuzingatia masharti
yaliyowekwa na kutoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Kaimu Katibu mtendaji wa
NACTE, Dkt.Adolf Rutayuga, alisema kuwa wamekuwa
wakifuatilia
vyuo vya ufundi ili kutathmini kama vinafuata viwango vya ubora wa
kitaaluma vilivyowekwa na NACTE katika kutoa mafunzo.
“Kama
ilivyoelezwa katika sheria za Usajili na Kanuni za leseni, kutozingatia
matakwa yoyoye yaliyowekwa na NACTE ni kosa kisheria. Kanuni zinasema
kuwa hatua kali zinawezakuchukuliwa kwa kila kosa. Kulingana na matokeo
ya ufuatiliaji uliofanywa na timu maalumu, Baraza lina uwezo wa
kuchukua hatua dhidi ya taasisi au vyuo vinavyoshindwa kutekeleza kanuni
zilizowekwa,” alisema.
Alisema
kuwa baada ya kufanya utafiti wao, wamebaini vyuo 26 vilishindwa
kuzingatia masharti yaliyowekwa na NACTE katika
cheti cha usajili, huku vyuo 20 vikitoa mafunzo ambayo
hayajathibitishwa chini ya idara isiyotambulika,wakati vyuo viwili
vikiwa na vituo vya satellite/Kampasi ambavyo navyo havijathibitishwa na
chombo husika.
“Baraza
linaufahamisha umma kwamba limechukua hatua mbalimbali kwa vyuo vya
ufundi 48 kutokana na makosa mbalimbali, yaliyofanywa na vyuo hivyo
ambapo limesitisha vyeti vilivyotolewa kwa vyuo 20 ambavyo vimeshindwa
kuzingatia masharti yaliyowekwa kwenye Cheti cha Usajili.
“Uamuzi huu umefanywa kwa mujibu wa Kanuni ya 20 ya Usajili wa Vyuo vya Ufundi ya mwaka 2001,” alisema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...