Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba, ambaye yuko Nairobi kuhudhuria kikao cha Bunge la Afrika Mashariki, ametumia fursa hiyo kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya na kuzungumza na watumishi.Katika kikao na Mhe. Waziri, watumishi wa Ubalozi walielezea changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika utendaji wa kazi, ikiwa ni pamoja na ufinyu wa bajeti. 

Hata hivyo watumishi hao walisema wameweza kukusanya maduhuli ya kuridhisha na kuhudumia Watanzania wanaopatwa na matatizo kwa kuchangishana wakati mwingine.Mhe. Kolimba alieleza kuridhishwa kwake na utendaji wa watumishi wa Ubalozi wa Nairobi na kuwapongeza kwa moyo wa kujitolea. 

Alisema Serikali itajitahidi kupatia balozi fedha na vifaa vya kazi kwa kadri ya uwezo wake, lakini akasisitiza watumishi wawe wabunifu na wajitolee kufidia pale upungufu unapojitokeza.Kikao cha Bunge la Afrika Mashariki kinachofanyika kwenye Bunge la Kenya kinatarajiwa kumalizika kesho.
Baadhi ya watumishi wa Ubalozi wakijipanga kumpokea Mhe. Naibu Waziri
 Mhe. Kolimba akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Ubalozi.
 Naibu Waziri, Dkt. Kolimba (kushoto) akifurahia bidhaa za Tanzania kwenye ofisi za Ubalozi wa Nairobi akiwa na Kaimu Balozi, Bi. Talha Mohamed Waziri. 
Naibu Waziri akiongea na watumishi wa Ubalozi. Kushoto ni Kaimu Balozi, Bi. Waziri na Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. James Lugaganya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...