NDEGE iliyokuwa imebeba watu 81, wafanyakazi tisa na abiria 72 ikiwemo timu ya soka ya klabu ya Chapecoense ya Brazil imeanguka katika sehemu ya milima nchini Colombia wakati inakaribia Mji wa Medellin na kuua watu 76 huku watano pekee wakinusurika.
Ndege hiyo ya kukodisha iliyokuwa ikitokea Bolivia, ilikuwa na timu ya soka ambayo ilikuwa icheze katika fainali ya Kombe la Amerika ya Kusini dhidi ya timu ya Atletico Nacional ya Medellin. Hivyo, fainali hiyo imeahirishwa.
Ripoti zinasema ndege hiyo yenye leseni namba CP 2933, ilianguka saa 4:15 jana usiku baada ya kupata hitilafu katika mfumo wake wa umeme na ilielezewa na Meya wa Medellin, Federico Gutierrez, kama “janga kubwa”, huku akiongeza kwamba inawezekana kuna watu walionusurika.
Imeelezwa kuwa baada ya ajali ndege hiyo ilivunjika katika vipande viwili na kupelekea vifo vya watu 76 huku watano pekee wakinusurika wakiwemo wachezaji watatu wa Chapecoense ambao ni beki Alan Ruschel, makipa Danilo Padilha na Jacson Follmann pamoja na abiria wengine wawili Rafael Correa Gobbato na Ximena Suarez.
Baadhi ya picha zilizowekwa mitandaoni zinawaonyesha wachezaji ambao hawakusafiri na timu hiyo wakiwa na simanzi katika vyumba vya kubadili nguo.

 Kabla ya kuanza safari timu hiyo ilipiga picha hizi.
 Kabla ya kuanza safari timu hiyo ilipiga picha hizi.

Wachezaji ambao hawakusafiri na timu hiyo wakiwa na simanzi katika vyumba vya kubadili nguo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...