Hussein Makame, NEC

TUME ya Taifa ya Uchaguzi imesema haitasita kuifutia kibali cha kutoa Elimu ya Mpiga Kura Asasi yoyote itakayotoa maneno ya kuleta uchochezi au kupigia debe sera za chama fulani cha siasa kwani kufanya hivyo kukiuka matakwa ya Kisheria.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Emmanuel Kawishe wakati akijibu swali la mmoja wa wajumbe wa mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma leo.

Mjumbe huyo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Mhandisi Stela Manyanya alitaka kufahamu Tume ina utaratibu gani kuhakikisha baadhi ya Asasi zinazofadhiliwa kutoa elimu ya mpiga kura kutumia nafasi hiyo kuhasisha sera za chama fulani.

Bw. Kawishe alisema Kifungu cha 4 (C) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kimeipa mamlaka Tume kuzipa kibali Asasi na kuzisimamia na kuratibu Elimu ya Mpiga Kura na haitasita kufuta kibali hicho iwapo masharti yatakiukwa. 
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) akimkaribisha ofisini kwake Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (wa pili kushoto) wakati kabla ya kutoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Wa pili kulia ni Katibu Tawala wa mkoa huo Bw. Hassan Bendeyeko na kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe. 
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (kulia) akieleza jambo wakati akitoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge na katikati ni Katibu Tawala wa mkoa huo Bw. Hassan Bendeyeko. 
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa NEC Bw. Emmanuel Kawishe, akitoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. 
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Mhe. Jaji Mstaafu Mary Longway (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Dkt. Binilith Mahenge vitabu vya Taarifa ya Tathmini Baada ya Uchgauzi wa Rais,Wabunge na Madiwani baada ya kutoa elimu ya mpiga kura kwenye mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. 
Baadhi ya wajumbe wa mkutano wa kamati ya Ushauri ya mkoa wa Ruvuma  uliofanyika kwenye halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wakifuatilia elimu ya mpiga kura. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...