Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) limeziagiza Kampuni ya simu nchini kutekeleza Sheria ya Fedha ya mwaka 2016 inavyotaka kuanza uandikishaji wa umikilikishaji wa asilimia 25 ya hisa zake kwa umma kwa kujiunga na soko la hisa la Dar es Salaam.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi.Beng’i Issa leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari.Amesema kuwa lengo la mabadiliko hayo ya kisheria katika sekta ya mawasiliano ni kuongeza uwazi katika usimamizi wa Kampuni hizo na kuongeza makusanyo ya kodi kwa Serikali.Bi. Beng’i ameongeza kuwa hatua hiyo itatoa fursa ya kuwawezesha watanzania kiuchumi kuwa wamiliki wa Kampuni hizo kupitia ununuaji wa hisa katika soko la hisa la Dar es Salaam.

“Kampuni za simu za mikononi hapa nchini zitakiwa kutekeleza mabadiliko haya ya kisheria ndani ya muda wa miezi sita kuanzia Julai Mosi mwaka huu kukamilisha taratibu za kisheria za masoko ya mitaji na hisa kwa kutoa asilimia 25 ya hisa zao na kujiunga na soko la hisa la Dar es salaam ili wananchi waweze kununua hisa kwa ajili ya kuwa sehemu ya wamiliki wa Kampuni hizo hapa nchini” alisisitiza Katibu Mtendaji huyo.

Aidha Katibu Mtendaji huyo ametoa wito kwa watanzania wote kujiandaa kushiriki kikamilifu katika ununuzi wa hisa za Kampuni hizo za simu mara zitakapokamilisha taratibu za kujiunga na soko la hisa la Dar es Salaam.

Mbali na hayo Baraza litatoa elimu kwa umma kwa muda wa mwezi mmoja kupitia vyombo mbalimbali vya habari katika kuelimisha na kuhamasisha umma kuhusu fursa hii muhimu kiuchumi na pia wananchi wataelimishwa namna ya kununua hisa,faida za kununua hisa pamoja na athari zake.

Baraza la Taifa la Uwezeshaji linatoa rai kwa Mashirika ya Hifadhi ya Jamii Nchini kuandaa utaratibu mzuri utakaowawezesha wanachama wao kuweza kushirika katika kununua hisa za Kampuni za si Aidha linafuatilia kwa karibu maendeleo ya utekelezaji wa mabadiliko haya ya kisheria na kuhakikisha utekelezaji wake unafanyika kwa wakati kama ilivyoainishwa katika sheria ya Fedha ya Mwaka 2016.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha mswada wa Sheria ya Fedha ya Mwaka 2016(The Finance Act, 2016) Juni, 23 mwaka huu ambapo pamoja na mambo mengine lilifanyia mabadiliko sheria ya electroniki na mawasiliano ya posta(Electronic and Postal Communication Act,Cap 306).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...