Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa leo amefanya ziara ya kutembelea Miradi mbalimbali ya Kuboresha Miundombinu ya Usambazaji umeme jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Miongoni mwa miradi aliyoitembelea ni Kituo cha Usambazaji Umeme Ilala kinachojengwa chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA), Mradi wa Kuboresha Huduma ya Umeme Katikati ya Jiji la Dar es Saalam katika Kituo cha Dar es Salaam City Centre na Mradi wa Kituo cha Kudhibiti Mifumo ya Usambazaji umeme, kilichopo eneo la Mikocheni Jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kutembelea miradi hiyo, Prof. Ntalikwa amesema kuwa, kukamilika kwake kutaimarisha miundombinu ya usambazaji umeme Jijini Dar es Saalam na hivyo kuwezesha Jiji la Dar es Salaam kupata umeme wa uhakika.

Akizungumzia kituo cha Kudhibiti Mifumo wa Usambazaji Umeme cha Mikocheni, kilichojengwa na Serikali ya Finland na Tanzania ameeleza kuwa, kituo hicho kimefungwa mashine za kisasa zinazotumia teknolojia za hali ya juu kama zinazotumiwa katika nchi zilizoendelea na hivyo, kukamilika kwake kutawezesha kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme jijini Dar es Salaam ikiwemo kubaini kwa haraka na moja kwa moja eneo lolote lenye hitilafu kupitia mitambo hiyo na hivyo kuwezesha tatizo kushughulikiwa kwa haraka.

“ Kwa ujumla nimeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya kuboresha miundombinu ya umeme inayotekelezwa jijini Dar es Salaam. Mradi wa Kuboresha Huduma ya Umeme Katikati ya Jiji la Dar es Saalam, unatarajiwa kuzinduliwa tarehe 16 Novemba,2016 na Mhe. Rais Dkt.John Magufuli. Kukamilika kwake kutakuwa na manufaa makubwa kwa upatikanaji umeme jijini Dar es Salaam,” ameongeza Prof. Ntalikwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba (kulia), akimwongoza Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa na ujumbe wake kutembelea maeneo mbalimbali katika Kituo cha Ilala, jijini Dar es Salaam, wakati wa ziara yake. 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa (wa kwanza kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba (katikati) wakati alipotembelea Mradi wa Kituo cha Kuboresha Miundombinu ya Umeme cha Ilala, jijini Dar es Saalam. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa na ujumbe aliofuatana nao, wakisikiliza maelezo ya kuhusu namna kituo cha Kudhibiti Mifumo wa Usambazaji Umeme cha Mikocheni, kinavyofanya kazi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...