Mkurugenzi  Mtendaji wa Hospitali ya Taifa  Muhimbili- MNH,  Profesa   Lawrence Museru amewataka wauguzi kufanya kazi kwa bidii  na kuzingatia maadili  ya Uuguzi ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa wanaofika kupata huduma  katika hospitali hiyo.

Profesa Museru  ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es salaam  katika  mkutano  wa wauguzi  Tawi la Muhimbili  uliolenga kumpongeza  kwa kuteuliwa  kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo .

Profesa Museru  amesema  licha ya  wauguzi hao kukabiliwa changamoto mbalimbali  lakini hawanabudi kufanya kazi kwa bidii na kuonyesha upendo kwa wagonjwa  ili kukabiliana na ushindani na kutoa huduma  bora.

“ Hii ni hospitali ya Taifa inatoa huduma za kibingwa hivyo ni lazima huduma zitolewe kwa kiwango cha juu kulingana na hadhi yake” amesema Profesa Museru.

Akisoma Risala kwa niaba ya wauguzi  Katibu wa TANNA  Taifa  Sebastian Luziga   amesema wauguzi wa MNH  wanamshukuru Profesa Museru kwa jinsi anavyojitoa kuwasaidia katika mambo mbalimbali  na kwamba  hali hiyo inaonyesha anathamini taaluma ya uuguzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Profesa Lawrence Museru akizungumza na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili katika mkutano uliofanyika leo hospitali hapo.
Baadhi ya wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimsikiliza kwa makini Profesa Museru katika mkutano ulioandaliwa na Chama cha Wauguzi  Tawi la Muhimbili .
Mkurugenzi wa Huduma ya Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Agnes Mtawa akimkabidi tuzo Profesa Museru kwa lengo la kumshukuru na kutambua mchango anaotoa kwa wauguzi wa hospitali hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...