Kampuni inayotoa huduma ya usafirishaji wa anga hapa nchini Qatar
Airways kwa miongo kadhaa sasa, kupitia safari zake za Dar es Salaam, Kirimanjaro na
Zanzibar imechangia madawai 100 katika shule ya msingi Chanzige B, iliyopo wilayani Kisarawe jijini Dar
es Salaaam. Hiyo ikiwa ni sehemu ya mradi wa kusaidia juhudi za serikari kupitia mpango wa kuondoa
uhaba wa madawati nchini kwa shule za Msingi pamoja na Sekondari, lakini pia wakiwa kama sehemu
ya kurudisha shukrani kwa jamii.
Makabidhianao hayo yamefanyika katika viwanja vya shule ya Chanzibe B,ambayo yalihudhuriwa na viongozi
mbalimbali, akiwemo Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo, Meneja wa Qatar Airways Tanzania, Basel Haydar, pamoja na wafanyakazi wa
Qatar Airways na wawakilishi kutoka ofisi ya Doha pamoja na Daktari Amon Mkoga, Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Amon Mkoga Foundation, Bodi ya wakurugenzi na walimu wa shule ya msingi
Chanzige B.
Wakati wakikabidhi mchango huo wa madawati, Meneja wa Qatar Airways Tanzania Basel Haydar, amemueleza Naibu
Waziri kuwa Qatar Airways itaendelea na mpango wa kusaidia jamii kwa kushirikiana na Serikali katika
kuinua na kuimarisha sekta ya elimu nchini.
Akiongea baada ya kupokea madawati hayo, Naibu Waziri Jafo ameipongeza kampuni
ya Qatar Airways kwa msaada wanaouonyesha, “Nawapongeza Qatar Airways kwa msaada huu, hii
inaonyesha wazi kuwa ni jinsi gani wanavyothamini elimu ya watoto wetu na mazingira kwa ujumla,
ambayo yanajumuisha madawati haya waliyokabidhi.
Elimu nzuri ndiyo itakayopeleka kizazi chetu katika
uzalishaji mkubwa na kukuza uchumi wa nchi yetu”
Mwalimu Mkuu wa Chanzige B, Pius Karinga, ametoa shukurani kwa kusema kuwa
“Tunaamini maboresho ya shule na mazingira ya kazi kwa Walimu nchini ni chachu ya kuongeza ufanisi
wa kuimarika kwa Mwanafunzi ambaye atakuwa na uwezo imara na kuwa sehemu ya uzalishaji muhimu
wa rasilimari watu nchini, hivyo basi tunatoa shukrani zetu zadhati kwa Qatar Airways kwa mpango wao
wa kuboresha mazingira yetu”.
Qatar Airways ilichagua kushirikana na Daktari Amon Mkonga Foundation katika kusaidia sekta ya elimu
nchini kwa kuwa wafanyakazi na sekta zingine mbalimbali wamepatikana kutokana na mazingira mazuri
ya kujifunzia. Hivyo msaada uliotolewa leo ni sehemu ya kuisaidia na kuzalisha kiwango kikubwa cha
rasilimali watu katika sekta mbalimbali hapo baadae.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...