Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka sawa mkono wenye drip wa mkewe Mama Janeth Magufuli, ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016.
Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na mkewe Mama Janeth Magufuli ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016. Kulia ni Dkt Edward Ngwale akiwa na wauguzi katika wodi hiyo. 
 : Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimjulia hali Waziri wa Zamani Balozi Omar Ramadhani Mapuri ambaye amelazwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwashukuru na kuwapongeza kwa kazi nzuri baadhi ya madaktari na wauguzi kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipotembelea wagonjwa pamoja na mkewe ambaye anapatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016.
Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwafariji baadhi ya wagonjwa kwenye wodi ya Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipotembelea kuona wagonjwa pamoja na mkewe ambaye anapatiwa matibabu hapo leo Novemba 10, 2016. 
Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipungia wananchi alipokuwa akitoka  Sewa Haji katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam alipotembelea wagonjwa pamoja na mkewe ambaye anapatiwa matibabu leo Novemba 10, 2016.
Picha na IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ajabu kweli kweli! Huyu Mama yeye anatibiwa nchini? Hajapekekwa Ulaya? Mungu Mbariki Magufuli. Mungu Ibariki Tanzania. Tunamuombea Mgonjwa pia.

    ReplyDelete
  2. Mungu akutie nguvu upone vizuri mama yetu, tunakupenda.

    ReplyDelete
  3. This is leadership by action. Sio wengine wafunge mikanda viongozi ule ule! Tofauti ya matendo ya viongozi na maneno yao ndo yamempatia Bwn Trump ushindi. Huyu Rais amejileta karibu na watu. Ameonyesha uongozi wa kweli. Wacha Wabunge wangang'anie mishahara yao Dodoma wanasaidia kuvijennga vyama vya akina Zitto tu. The should take a leaf from Magufuli's humility.

    ReplyDelete
  4. Kweli huyu ni raisi wetu anaongoza kwa vitendo.
    Mungu akubariki raisi wetu na nawapa pole wangonjwa wote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...