Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 26 Novemba, 2016 ametunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi 194 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  kundi la 59/15 katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Hii ni mara ya kwanza kwa Maafisa Wanafunzi wa JWTZ kutunukiwa Kamisheni nje ya Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kilichopo mkoani Arusha, na ni mara ya kwanza kwa Maafisa Wanafunzi wa JWTZ kutunukiwa Kamisheni ndani ya  Ikulu.

Maafisa hao ambao 168 ni wanaume na 26 ni wanawake, wametunukiwa Kamisheni katika cheo cha Luteni Usu na sasa wamekuwa Maafisa Wapya wa JWTZ.

Kabla ya kutunuku Kamisheni, Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli amekagua gwaride rasmi lililoandaliwa na Maafisa wanafunzi wa JWTZ na baadaye akashuhudia uhodari wa askari kutoka kikosi cha maadhimisho cha JWTZ waliofanya onesho la gwaride la kimyakimya.

Akizungumza baada ya chakula cha mchana katika ukumbi wa Ikulu, Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange, Makamanda na Askari wote wa JWTZ kwa jukumu kubwa wanalolitekeleza la kuhakikisha nchi ipo salama na amesema Serikali itahakikisha inaboresha zaidi maslai na mazingira ya kazi kwa Jeshi hilo na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.

Aidha, Rais Magufuli amesema ameamua tukio hili la kutunuku Kamisheni lifanyike Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa heshima kwa Maafisa wa JWTZ kama ambavyo Viongozi wengine Serikalini wamekuwa wakipata heshima ya kuapishiwa Ikulu.

"Kwamba Mawaziri tunapotaka kuwaapisha tunawaapishia hapa, Wakuu wa Mikoa tunawaapishia hapahapa, Makatibu Wakuu tunawaapishia hapahapa, kwa nini hawa Maafisa wa Jeshi tusiwaapishie hapahapa kwenye nyumba yao? Nyinyi ndio mnalinda nchi, nyinyi ndio mnasimamia usalama wa nchi hii, lakini nikiuliza hapa inawezekana wengine mpaka wamekuwa Mabrigedia Jenerali hawajawahi kukanyaga Ikulu, wakati hapa ni kwenu" amesema Rais Magufuli.

Sherehe za kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi hao zimehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na Wakuu wa Jeshi la Ulinzi wastaafu na Majenerali wastaafu wa JWTZ.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

26 Novemba, 2016
  Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitunuku kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  Novemba 26, 2016
 :Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua gwaride la heshima linaloundwa na Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es  salaam  Novemba 26, 2016


 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kwenye hati  ya  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kwenye hati  ya  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea baada ya kutunuku  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea baada ya kutunuku  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016.  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Dr. JPM, ukaguzi wa vyeti duni na utumiaji wa vyeti vya ndugu ningeomba ukapita kwenye majeshi yoote. hili tatizo lipo sugu mno. Tutakuja shindwa vita kwa kuwapa ajira muhimu watu wasiostahili. swala siyo eti nao wapate maisha au wataishije bila kazi, swala ni usalama wa nchi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...