RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amewataka wahitimu wa vyuo vikuu nchini kuacha tabia ya kuchagua kazi za kufanya mara baada ya kuhitimu elimu yao. Mwinyi alisema tabia hiyo imepitwa cha wakati hasa katika dunia ya sasa yenye changamoto kubwa ya ajira.
Rais Mwinyi alitoa
kauli hiyo juzi wakati akizungumza na wahitimu wa kozi mbalimbali
kwenye sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU)
cha jijini Dar es Salaam.
Alisema kitendo
cha baadhi ya wahitimu hasa wa vyuo vikuu kupendelea kuchagua kazi za kufanya
kimekuwa kikiwapotezea muda na fursa anuai, hivyo kuwataka kuacha tabia hiyo
ambayo kwa kipindi hiki imepitwa na wakati.Alisema wahitimu
hawana budi kuanza kufanya kazi zozote zinazojitokeza mbele yao na kutumia
fursa hiyo kuelekea kwenye mafanikio kadri walivyojipangia katika maisha yao.
"...Nawapongeza
wahitimu kwa hatua hii, sasa mnaingia katika maisha mapya na ya vitendo msiende
kuchagua kazi za kufanya, anza na kazi yoyote inayojitokeza mbele yako kisha uitumie
kutimiza ndoto zako," alisema katika hotuba yake kwa wahitimu hao.
Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi akiwatunuku wahitimu wa kozi mbalimbali katika mahafali ya Chuo Kikuu cha Kampala cha jijini Dar es Salaam kwenye sherehe za mahafali.
Baadhi ya waadhiri wa chuo hicho wakiwa kwenye mahafali hayo.
Baadhi ya wahitimu wa ngazi ya digree kozi ya afya wakila kiapo cha kuhitimu fani hiyo.
Sehemu ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo.
Msafara wa mahafali ukiongozwa na Rais msaafu wa Awamu ya Pili, Mwinyi mara baada ya sherehe za mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Kampala (KIU) cha jijini Dar es Salaam.kumalizika.
|
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...