Nteghenjwa Hosseah - Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo amezinduzaa daraja la Mto Kijenge linalounganisha kata za Engutoto na Moshono ambalo limejengwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Dharam Singh Hanspaul.

Akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa amesema daraja hilo ni ukombozi na msaada kwa wananchi wengi ambao walikua wakipata adha kubwa ya kuvuka haswa wakati wa mvua kutokana na kukosa kivuko cha uhakika na kivuko kilichokuwepo awali kiliashiria hali ya hatari kubwa kwa watoto, wazee, waendesha pikipiki, waenda kwa miguu wote na zaidi hakuna Gari lililokuwa na uwezo wa kupita hapo.

Hii ndio tunayoita kurudisha kwa jamii “Community Social Responsibility”, kampuni hii ya Hanspaul imetoa msaada ambao utatoa mchango mkubwa sana kwa jamii na sisi kama Serikali tunafarijika kwa kuona wadau wanaunga mkono jitihada za Serikaili kwa kiwango hiki hili ni jambo la kuigwa na Kampuni nyingine wajifunze katika hili.

Katika uzinduzi wa daraja hili Rc Gambo alitumia fursa hiyo alisikiliza kero za wananchi waliohudhuria na ambao wamelalamikia uuzaji holela wa maeneo ya wazi ya Serikali hali inayopelekea uhaba wa maeneo ya kujenga huduma za kijamii kama zahanati na shule huduma ambazo hazipatikani katika kata ya Engutoto hiyo hivyo wameiomba serikali itatue tatizo hilo ili wananchi wapate huduma bora za ijamii. 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizindua Daraja la Mto Kijenge.
Hili ndilo Daraja lililojengwa na wafadhili chini ya Bw. Hans Paul lina upana wa Mita 20, uwezo wa kupitisha magari yenye uzito wa Tani 3, urefu kwenda juu Mita 2.2 na uwezo wa kudumu kwa miaka 50. 
 Daraja walilokuwa wanatumia wananchi wa Engutoto na Moshono kabla ya kujengewa Daraja la kiwango na Kampuni ya Dharam Sign Hanspaul .

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(kwanza kulia) akipokea Kero kutoka kwa mwananchi kama zilivyowasilishwa na Mama Debora wakati wa  Unzinduzi wa Daraja la Mto Kijenge 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...