Vijana walio chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys wakiwasili katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa J.K.Nyerere tayari kwa safari kuelekea nchini Korea ya Kusini kushiriki mashindano maalumu ya vijana walio katika umri huo.
 Afisa Habari wa Shirikisho la Kabumbu Tanzania TFF,Alfred Lucas akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya timu ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys na viongozi 8 kuondoka jijini Dar es salaam leo kuelekea nchini Korea ya Kusini kushiriki mashindano maalumu ya vijana walio katika umri huo.

Vijana walio chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys akiingia kwenye eneo la ukaguzi katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa J.K.Nyerere tayari kwa safari kuelekea nchini Korea ya Kusini kushiriki mashindano maalumu ya vijana walio katika umri huo. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.


Na Dacpopo wa Globu ya jamii,

Kikosi cha wachezaji 19 wa timu ya vijana walio chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys na viongozi 8 wamondoka jijini Dar es salaam leo kuelekea nchini Korea ya Kusini kushiriki mashindano maalumu ya vijana walio katika umri huo.

Akizungumza baada ya kuwaaga wachezaji hao katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa J.K.Nyerere afisa habari wa shirikisho la kabumbu Tanzania TFF Alfred Lucas alisema kuwa mashindano hayo yanayojumuisha mataifa manne yameandaliwa na shirikisho la kandanda la Korea ya Kusini na kupewa baraka na FIFA.

Amesema kuwa hiyo ni nafasi nzuri ya mazoezi kwa timu hiyo kwani iwapo rufaa iliyokatwa na TFF kuhusu timu ya taifa ya Congo ya umri huo kumchezesha mchezaji aliyezidi umri timu hizo zilipopambana kuwania kushiriki mashindano ya Afrika itafaulu basi timu yetu itakuwa imepata mafunzo ya kutosha na kujiweka vizuri zaidi kwa fainali hizo zitakazofanyika Madagaska.

Wakati huo huo Alfred Lucas amesema kuwa timu yoyote iliyo katika Ligi Kuu ya kandanda nchini VPL ambayo haitapeleka timu yake ya vijana wa chini ya umri wa miaka 20 katika mashindano yake yatakayofanyika katika vituo vya Kagera na Dar es salaam itakumbwa na adhabu ya faini na kunyang’anywa pointi.

Ametanabaisha kuwa kutokana na kanuni ya 42 kifungu cha 27 ya kanuni za ligi timu ikikosa mchezo wa kwanza itapokwa pointi 3 na faini ya sh.2,000,000/ na kama haitapelka timu basi timu yake kubwa itapokwa pointi 12 kutoka katika pointi ilizonazo kwenye msimamo wa ligi ulivyo sasa.

Ametoa kauli hiyo kufuatia klabu za Yanga na African Lion kutishia kutopeleka timu zao za vijana katika kituo cha Kagera ambazo wamepangiwa,mashindano hayo yamepangwa kuanza tarehe 16 ya mwezi huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...