Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo (wa Tatu kulia) akiwa katika
mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka uliopo kata ya Ruanda mkoani Ruvuma ambapo aliambatana na watendaji mbalimbali kutoka
viwanda vya simenti vinavyotumia makaa ya mawe, Chama cha Wamiliki wa Malori
(TATOA), Wazalishaji wa Makaa ya Mawe, Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini
na viongozi kutoka Mkoa wa Ruvuma.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter
Muhongo (wa tatu kushoto) akipata maelezo kuhusu briketi za makaa ya mawe
zinazotengenezwa na kikundi cha Wanawake cha Mbarawala kwa ajili ya kupikia. Kikundi kinafadhiliwa na kampuni ya TANCOAL
inayomiliki Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Ngaka ulipo mkoani Ruvuma. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mbinga
Cosmas Nsheye, wa pili kushoto ni Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Ally
Samaje. Anayetoa maelezo ni Meneja Uendeshaji wa Kikundi hicho, Hajiri Kapinga. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...