Hayo yamesemwa jana na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi wakati akihojiwa na kipindi maalumu cha TUNATEKELEZA kinachorushwa hewani na kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC1).


Meja Jenerali Milanzi anasema Serikali imeweka mfumo maalumkatika kulinda hifadhi zilizopo na ili kuweza kukabiliana na ujangili unaojitokeza katika hifadhi mbalimbali nchini.

“Sekta ya Utalii nchini inachangia pato la taifa kwa takribani asilimia 17.5 na kutoa ajira kwa zaidi ya watumishi milioni 3 katika sekta mbali mbali ya utalii nchini, hivyo ni vyema tukaweka mikakati madhubuti katika kulinda vyanzo vilivyopo” alisema Meja Milanzi.

Aidha, alisema kuwa Serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria watu wote watakaobainika kujihusisha na ujangili pamoja na biashara ya magogo ili kulinda hifadhi za Taifa na kuweza kuvutia watalii nchini.Aidha Meja Jenerali Milanzi aliitaka jamii kwa ujumla kuona umuhimu wa kutumia nishati mbadala ili kulinda misitu iliyopo kwa kutunza mazingira na hifadhi za taifa.

Mbali na hayo Meja Jenerali Milanzi alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazovutia watalii wengi kutoka Marekani na Uingereza hivyo kuwataka wananchi kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamimia Hifadhi za Taifa ili kuzudi kuvutia watalii nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...