Serikali imeahidi kutenga jumla ya Dola za kimarekani Millioni 115 kwa ajili ya kuboresha lishe ikiwa ni mpango wa maendeleo wa miaka mitano 2016/2021 na mkakati wa kuboresha lishe kwa mwaka 2016/2021.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipokuwa akizungumza katika halfa ya kuwatunuku tuzo waandishi bora wa habari zinazohusu lishe iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Anastazia Wambura ameongeza kuwa bado kumekuwa na changamoto katika upatikanaji wa lishe bora nchini ikiwemo kuwepo kwa tamaduni mbalimbali zinazonyima fursa kwa watoto na wakina mama kuoata lishe iliyo bora.

“Serikali imeingiza suala la lishe katika mpango wa maendeleo wa taifa wa miaka mitano na katika kulitekeleza hili Serikali ya awamu ya Tano itatenga dola million 115 kwa ajili ya mkakati wa kuboresha lishe nchini” alisisitiza Mhe. Anastazia.

Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikabidhi cheti zawadi ya tablet na Shillingi million 1.5 kwa Bi Tumaini Msoyowa mshindi wa kwanza wa Shindano la mwandishi bora wa habari zinazohusu lishe kutoka gazeti la Mwananchi katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikabidhi cheti zawadi ya tablet na Shillingi million 1 kwa mwakilishi wa Bi Winny Itaeli wa mshindi wa pili wa Shindano la mwandishi bora wa habari zinazohusu lishe kutoka gazeti la The Guardian katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akikabidhi cheti na Shillingi laki 5 kwa Bw. Gerald Kitabu mshindi wa tatu wa Shindano la mwandishi bora wa habari zinazohusu lishe katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.
Baadhi ya Washiriki wa shindano la mwaandishi bora wa habari za masuala ya lishe pamoja na wageni waalikwa wakifuatilia hotuba mbalimbali ikiwemo ya Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura wakati wa hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam Novemba 22,2016.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...