Serekali imewataka Waratibu wa Uwezeshaji wa Wizara walioteuliwa kuwa watendaji makini ili kusaidia kamati zao za uwezeshaji wananchi kufuatilia kwa ukamilifu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mwaka 2004 na kuchangia kuandaa takwimu za uchumi wa taifa.

Akifungua mafunzo ya siku tatu ya Wenyeviti wa Kamati za Uwezeshaji na Waratibu wa Uwezeshaji, mjini hapa jana, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde, amesema kuwa sababu ya serekali kuwa na kamati na waratibu hao ni kupata watendaji wa kutumikia Watanzania kwa kuwawezesha, kuwasaidia kumiliki kikamilifu na kunufaika na uchumi wa taifa katika mazingira ya sasa.

Waziri huyo ameliita suala la uwezeshaji wananchi kuwa ni ajenda muhimu ya taifa na kutaka zikusanywe takwimu za kuridhisha juu ya ukuwaji wa uchumi katika miaka na jinsi wananchi wanavyonufaika na ukuwaji huo. Amesisitiza “..haitakuwa na maana kama ukuwaji wa uchumi hauwanufaishi wananchi walio wengi na (pia kama) hazipo takwimu za kuridhisha za ukuaji wa chumi.”

Akisisitiza umuhimu wa ufuatiliaji, waziri amesema maeneo ya kupwewa kipaumbele ni kujua ni kiasi gani Watanzania wanashiriki na kunufaika kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa hapa nchini na makampuni ya kigeni katika sekta mbali mbali.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde ((katikati) akisisitiza jambo wakati akifungua mafunzo ya siku tatu ya Wenyeviti wa Kamati za Uwezeshaji na Waratibu wa Uwezeshaji, mafunzo yenye lengo la kuwajengea uwezo wa uwelewa na wajibu wao katika Wizara, Idara na Taasisi mbalimbali wanazotoka (kulia) ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel, (kushoto) ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ( NEEC) Bi. Beng’i Issa.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde (kushoto) akimsikiliza kwa makini ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel ( kulia) muda mfupi mara baada Naibu Waziri huyo fungua mafunzo ya siku tatu ya Wenyeviti wa Kamati za Uwezeshaji na Waratibu wa Uwezeshaji, mafunzo yenye lengo la kuwajengea uwezo wa uwelewa na wajibu wao katika Wizara, Idara na Taasisi wanazotoka, Morogoro jana, (katikati) ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ( NEEC) Bi. Beng’i Issa.
Baadhi ya Wenyeviti wa Kamati za Uwezeshaji na Waratibu wa Uwezeshaji wakifuatilia mafunzo ya siku tatu ya Wenyeviti wa Kamati za Uwezeshaji na Waratibu wa Uwezeshaji, mafunzo yenye lengo la kuwajengea uwezo wa uwelewa na wajibu wao katika Wizara, Idara na Taasisi wanazotoka, mafunzo hayo yalifunguliwa jana Mkoani Morogoro na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira Mh. Anthony Mavunde.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...