Na Lucas Mboje, Jeshi la Magereza Dar es Salaam
KAMISHNA Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, John Casmir Minja
amekutana na Wawekezaji wa Kampuni ya CAMCE kutoka nchini China
pamoja na Kampuni ya Wazawa ya KG CORPORATION na kumuahidi
kushirikiana na Shirika la Uzalishaji Mali la Magereza(Prisons Corporation
Sole) katika kuwekeza katika miradi mbalimbali ya Kilimo cha kisasa, Madini
na Viwanda vinavyoendeshwa na Shirika hilo.
Akizungumza na Wawekezaji hao leo asbuhi Ofisini kwake (Jumatano,
Novemba 2, 2016) alisema kwamba Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la
Uzalishaji mali lina fursa nyingi za miradi ya uwekezaji kwenye sekta nyingi
kama vile Kilimo, Viwanda na Madini ambapo aliwahahakishia ushirikiano wa
kutosha kwenye uwekezaji wao.
Wawekezaji hao tayari wamefanya mazungumzo na Viongozi wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo wanatarajia kuiingia Makubaliano (MoU) na
Jeshi la Magereza kwa ajili ya miradi mbalimbali ikiwemo ya Kilimo cha
kisasa katika Gereza Idete lililopo Mkoani Morogoro pamoja na Mradi wa
Ngo’mbe wa nyama Gereza Ubena, Mkoani Pwani.
Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya
CAMCE kutoka nchini China Bw. Lane Lei alisema amefurahishwa na ziara
waliyofanya nchini na wapo tayari kuwekeza hapa Tanzania.
Naye, Mwakilishi wa Kampuni ya Wazawa ya KG CORPORATION Bw. Dan
Ngowi ambayo inashughulikia na masuala ya Kilimo cha mazao ya chakula na
nyama alisema watawekeza kwenye kilimo hususan cha umwagiliaji na
watajenga Kiwanda kwa ajili ya usindikaji.
Shirika la Uzalishaji mali la Magereza(Prisons Corporation Sole) lina jumla
ya Miradi 23, kati ya hiyo miradi 15 ni ya kilimo na mifugo na 8 ni ya viwanda
vidogo vidogo, pia zipo shughuli za mradi wa Kikosi cha Ujenzi
zinazosimamiwa na Shirika hilo.
Mkakati wa Jeshi la Magereza hivi sasa ni kuendelea kuboresha maeneo
mbalimbali pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo ikiwemo uwekezaji wa
ubia kwenye miradi yake ili kuhakikisha kuwa linafikia ufanisi unaotarajiwa
katika utekelezaji wa majukumu yake.
Kamishna Jenerali wa Mgereza – CGP John Casmir Minja(katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na Wawekezaji wa masuala ya Kilimo cha
kisasa mara baada ya mazungumzo Ofisini kwake leo Novemba 2, 2016,
Makao Makuu ya Magereza(kulia) ni Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki
wa Kampuni ya CAMCE kutoka nchini China Bw. Lane Lei(kushoto) ni
Mwakilishi wa Kampuni ya Wazawa ya KG CORPORATION Bw. Dan Ngowi.
Safi sana, uwekezaji wa kampuni za wazawa zikishirikiana na wageni ndio utaleta tija katika PPP na parastatal za serikali
ReplyDelete