Baada ya kupokea ndege mpya aina ya Airbus mwezi wa tisa mwaka huu, Shirika la ndege la Rwandair limepokea tena ndege nyingine mpya aina ya Boeing 737-800 kizazi kipya yenye kubeba abiria 154.

Akizungumza kuhusu ndege hiyo, Meneja mkazi wa RwandAir hapa Tanzania, Ibrahim Bukenya amesema kuwa ujio wa ndege hii umetimiza idadi ya ndege 10 zilizonunuliwa na shirika hilo. 

Amesema kuwa kuanzia Disemba 8, 2016 shirika hilo litaongeza safari zake mara 14 kwa wiki badala ya sasa mara 11 kutokea Dar es Salaam kuelekea Kigali na kuunganisha Lagos, Accra, Abidjan, Cotonou, Libreville, Brazzaville, Douala, Kamembe, Lusaka, Johannesburg, Bujumbura, Entebbe, Nairobi, Mombasa, Dubai na Juba.
Bukenya ameendelea kusema kuwa Shirika hilo linategemea kuanzisha safari zake za kuelekea Harare, Bombay na London mwanzo mwa mwezi wa kwanza mwaka 2017.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...