Na Amina Kibwana- Globu ya Jamii.
Ofisi
ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na wadau mbalimbali leo
wameadhimisha siku ya takwimu afrika kwa lengo la kuongeza uelewa mpana
kwa watumiaji wote wa takwimu Afrika na kuhusu umuhimu wa Takwimu katika
kupanga mipango ya maendeleo katika sekta zote za kijamii na kiuchumi.
Mkurugenzi
mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dr.Albina Chuwa amesema kuwa faida za
kuwa na takwimu za kiuchumi katika mtengamano wa kikanda na miundo yake
kwa Nchi yetu ni wa muhimu sana hususan kwa wakati huu ambao serikari
yetu inapigania uchumi wa viwanda, Hivyo uboreshaji wa takwimu kwa
kutumia teknolojia ya kisasa ni jukumu shirikishi likiongozwa na Ofisi
ya Takwimu.
Chuwa
amesema kuwa kwa kutumia kauli mbiu hii "Kuimarisha Takwimu za kiuchumi
kwa Mtangamano wa Kikanda, Mabadiliko ya Miundo na Maendeleo Endelevu",
ambayo ilitolewa na Umoja wa jumuia ya Afrika kwa kushirikiana na Ofisi
ya takwimu Afrika itasaidia kuimarisha na kuboresha umuhimu wa takwimu
kwa ajili ya maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Akizungumza
kwa niaba ya Mgeni rasmi Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,
Jinsia ,Wazee na watoto,Dr.Khamisi Kigwangalla kuwa kauli mbiu ya mwaka
huu inaenda sambamba na Utekelezaji wa Malengo endelevu ya Maendeleo ya
Dunia ya mwaka 20130,Agenda ya Afrika ya mwaka 2063 na mpango wa pili wa
Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2016 na 2017 hadi 2020 na 2021 kwa lengo la
kukuza uchumi na kupunguza umaskini kwa Duniani, bara la Afrika na
Tanzania kwa ujumla.
Dkt.
Kingwagalla amesema kuwa umuhimu wa Takwimu za Uchumi haziwezi
kukwepeka, akaongeza kusema kuwa ni lazima Watakwimu na wachumi wote
ndani na nje ya Afrika na hususan hapa Nchini ambapo wana jukumu la
kuhakikisha wanatimiza wajibu wao waliotumwa na wananchi kwa kuleta
maendeleo ya kweli ndani ya Serikali ya Awamu ya tano yenye kauli mbiu
ya Hapa kazi tu.
"Kuwepo
kwa takwimu za kiuchumi zenye ubora kunasaidia sana katika kupanga
mipango bora ya kiuchumi na maendeleo ya jamii, hivyo basi tunahitaji
kuona takwimu za kiuchumi zinapatikana kwa wakati na zenye ubora
unaofuata kanuni zilizowekwa na ofisi ya Takwimu ya Umoja wa Mataifa na
kwa kutumia ubora wa uhakika".
Siku
ya takwimu Afrika imeanzishwa na Bodi ya Umoja wa Mataifa, Kamisheni ya
uchumi ya Afrika ( UNECA), Wachumi na watakwimu tangu mwaka 1990,
ambapo siku hii pia hutoa fursa kwa Nchi kutathmini na kufuatilia
malengo yaliyofikiwa katika Mipango ya Maendeleo ya ndani ya nje ya
nchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...