Mshambuliaji wa Timu ya African Lyon  Omary Abdallah akiwatoka mabeki wa Timu ya Simba, Novality LUfunga na Jonas Mkude, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. African Lyon imeshinda bao 1-0.

Timu ya African Lyon imefanikiwa kuondoka na alama tatu katika Uwanja wa Uhuru baada ya kuifunga Simba goli dakika ya 96 na kuweka rekodi ya kuwafunga wekundu hao wa Msimbazi toka ligi ianze.
African Lyon waliweza kucheza kwa makini na waliweza kutumiawaliitumia kwenye kipindi cha kwanza, ilizaa matunda kutokana na kuibana Simba ambayo ilionekana kushindwa kabisa kupenya safu ya ulinzi ya Lyon.

Pamoja na kujitahidi kutengeneza nafasi za mabao na kupata kona tatu kwenye kipindi cha kwanza, mashambulizi mengi ya Simba yaliishia mikononi mwa kipa Youthe Rostand wa Lyon ambaye alikuwa kikwazo kwenye mchezo huo.
Dakika nne za nyongeza kwenye mchezo huo, zilikuwa chungu kwa Simba baada ya mshambuliaji Abdallah Msuhi kuitumia vyema krosi Ya Rahidhan Hafidh na kuifungia bao Lyon ambalo limevunja rekodi ya Simba kucheza mechi 13 za ligi bila kupoteza.
Kufungwa kwa bao hilo kuliwachochea mashabiki wa Simba ambao walianza kurusha makopo ya maji uwanjani wakionyesha kutoridhishwa na mwamuzi wa pembeni Frank Komba wakidai kuwa mpigaji wa krosi alikuwa ameotea. 
 Mshambuliaji wa Timu ya African Lyon, Abdullah Msuhi akiachia shuti lililoingia moja kwa moja wavuni na kuiandikia timu yake bao la kuongoza dhidi ya Timu ya Simba, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. African Lyon imeshinda bao 1-0.
 Mshambuliaji wa Timu ya African Lyon, Abdullah Msuhi akiruka juu kushandilia goli lake dhidi ya Wekundu wa Msimbazi, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. African Lyon imeshinda bao 1-0.
 
Mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo akiichachafya ngome ya African Lyon. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...