Na Evelyn Mkokoi – Singida.

Katika kutekeleza agizo la Serikali la usafi wa mazingira kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi, wananchi wa Mkoa wa Singida wamejitokeza kwa kwingi katika zoezi hilo lililofanyika kitaifa mwezi huu mkoani humo.

Akishiriki zoezi hilo  Mkoani Singida kitaifa, Naibu waziri Ofisi ya Makamu w Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ameupongeza uongozi wa Mkoa wa Singida na wana  singida kwa ujumla kwa jitihada walizoonyesha kwani kila eneo la Singida Jumamosi ya leo Limeonekana kuwa nadhifu kabla hata ya muda wa kuanza kufanya usafi tofauti na mikoa mingine ambayo amewahi kushiriki zoeZi hilo.

Akiongea na Hadhara iliyojitokeza katika siku ya usafi Mjini Singida Leo, Mpina alisema kuwa usafi wa mazingira  unapunguza magonjwa yatokanayo na uchafu akitolea mfano ugonjwa wa kipindu pindu na hivyo taifa likiwa safi litaweza kuokoa ngumukazi yake, na kupunguza gharama ambazo zingetumika kutibu maradhi hayo.

“Ukiona Msichana mzuri barabarani ujue kagharamiwa ukiona kijana mtanashati vilevile ujue kagharamiwa Mkiona taifa zuri na safi ujue limegharamiwa na wananchi wake wamejipanga vizuri, hivyo wana singida Muendelee kujitahidi katika suala zima la usafiwa mazingira.” Alisisitiza Mpina.

Zoezi la usafi wa Mazingira Mkoani Singida lilienda sambamba na zoezi la upandaji miti ambapo, Naibu Waziri Mpina Pia alishiriki  na wananchi katika zoezi la kupanda miti mkoani Singida ambapo alipanda mti aina ya mpararachichi katika eneo la stand mpya ya Misuna.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Pamoja na wananchi wa Mji wa Singida wakikusanya uchafu katika siku ya Usafi Kitaifa Mjini Singida.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muugano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akipeleka uchafu katika kizimba cha uchafu cha soko  kuu la Singida lililoko katika Mtaa wa Ipembe.
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina akiandaa mche wa mti kitalam kabla ya kuupanda katika zoezi la usafi na upandaji miti mjini Singida leo.


Naibu Wazir Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina Akipanda Mti aina ya Mparachichi katika eneo la Misuna Stand Mpya Mjini Singida leo katika Zezi la usafi wa mazingira Kitaifa. (Picha na Evelyn Mkokoi wa OMR)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...