Mbunifu wa mitindo Mustafa Hassanali akizungumza na waandishi wa habari juu ya onesho la Swahili Fashion Week, kulia kwake ni katibu mkuu wa Baraza la Sanaa nchini(BASATA) , Godfrey Mwingereza.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

LILE tamasha maharufu la Mitindo la wiki (Swahili Fashion Week) limetangazwa rasmi kuanza kufanyika Desemba 2 mpaka 4 katika viwanja vya makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na muaandaaji na mratibu wa Tamasha hilo Mustafa Hassanal alipokuwa akizundua onyesho hilo katika Hotel ya Collesium jijini Dar es salaam.

“jukwaa hili linachukuliwa kuwa ni kiongozi katika suala la uvumbuzi na uoneshaji wa kazi za kibunifu hivyo watu kutoka nchi mbalimbali wanasubiri kwa hamu kuona onyesho hili la aina yake katika ukanda huu wa afrika mashariki”amesema Hassanal.

Amesema kuwa lengo la kuendeleza mitindo ya kiafrika bado lipo katika mstari wa mbele kupitia jukwaa hilo wabunifu wataweza kukuza thamani ya bidhaa zao.

Ametaja kuwa katika onesho la mwaka huu kutakuwa na jukwa kwa siku tatu mfulilizo kuanzia saa mbili na nus asubuhi huku watu wakiendelea kununua bidhaa mbalimbali zitakazo kuwepo hapo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...