Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi jana Novemba 15, 2016 alimtembelea Mstahiki Meya wa Jiji la Seongnam, Jae-myung Lee kumshukuru kwa namna ambavyo ameipokea timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys.

Serengeti Boys walioko Korea kwa michezo ya kirafiki ya kimataifa ambako Jiji la Seongnam ni mshirika wa klabu ya Seongnam FC ambao ndio wenyeji wa timu yetu ya vijana ambayo ilifanya michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

TFF YAMSIMAMISHA MCHEZAJI KAGERA SUGAR
Kutokana na malalamiko ya timu ya mpira wa miguu ya Panone Fc juu ya ushiriki wa mchezaji Christopher Mahanga katika Ligi ya TFF ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 iliyoko Kundi A, Kituo cha Bukoba Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limesimamisha ushiriki mchezaji Christopher Mshanga katika mashindano yanayoendelea mpaka uchunguzi wa suala lake utakapokamilika.

Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji italifanyia kazi suala hilo na taarifa itatolewa.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

BURIANI MSAFIRI RAMADHANI MSAFIRI
Shirikisho la Mpira wa Miguu wa Miguu Tanzania (TFF), limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA), Msafiri Ramadhani Msafiri.
Taarifa za kifo hicho kilichotokea usiku wa kuamkia Novemba 15, mwaka huu akiwa njiani kwenda Hospitali ya Milagwe, Kampala nchini Uganda, imetolewa na Katibu Mkuu wa KRFA, Saloum Chama ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji TFF.
Kwa taarifa zaidi, fuata link hapo chini

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...